Tuesday, May 8, 2012

SAFARI YA CHINA YAIVA KWA DROGBA.

MAWAKALA watatu wa mshambuliaji wa Chelsea, Didier Drogba wanatarajia kukutana na mmiliki wa klabu ya Shanghai Shenhua, Zhu Jun baadae leo kuangalia uwezekano wa uhamisho wa mshambuliaji huyo kwenda kwenye klabu hiyo. Kwa mujibu wa taarifa za gazeti la michezo la Sina la nchini humo limedai kuwa tajiri huyo anatarajiwa kukutana na mawakala hao nchini Singapore. Drogba mwenye umri wa miaka 34 kwa muda mrefu amekuwa akihusishwa na habari za kuhamia katika klabu hiyo wakati ambapo mkataba wake unaishia mwishoni mwa msimu huu. Kuna taarifa kuwa Drogba ambaye alifunga bao wakati timu yake ikiibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Liverpool katika Kombe la FA atakuwa akilipwa paundi 250,000 kwa wiki katika mkataba wa miaka miwili atakaopewa na klabu hiyo kama akikubali.

No comments:

Post a Comment