Thursday, May 24, 2012

MAN UNITED YAMTENGEA EURO MILIONI 13 KAGAWA.

KLABU ya Manchester United imeanza hekaheka za usajili baada ya kutangaza kutenga kiasi cha euro milioni 13 kwa ajili ya kumnasa Shinji Kagawa kutoka klabu ya Borussia Dortmund ya Ujerumani. United imeingia katika kinyang’anyiro hicho cha kumnasa kiungo huyo baada ya kupata taarifa kuwa klabu ya Arsenal nayo imeonyesha nia ya kuitaka saini ya mchezaji huyo. Katika taarifa zilizotolewa Alhamisi United walitangaza dau hilo baada ya Dortmund kuthibitisha kumuweka sokoni mchezaji huyo wa kimataifa wa Japan. United iliingia katika orodha ya timu zinazomyemelea mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 toka Aprili mwaka huu wakati ambapo Dortmund walitangaza kumwachia Kagawa katika kipindi cha usajili majira ya kiangazi.

No comments:

Post a Comment