Tuesday, May 8, 2012

IKPEBA AKANUSHA UVUMI WA KUMTENGA YEKINI.

MCHEZAJI wa zamani wa kimataifa wa Nigeria, Victor Ikpeba amekanusha uvumi uliozagaa kuwa baadhi wa wachezaji wa kikosi cha nchi hiyo kilichoshiriki michuano ya Kombe la Dunia mwaka 1994 nchini Marekani walikuwa wakimpinga Rashid Yekini. Yekini alifariki dunia Ijumaa iliyopita katika mji wa nyumbani kwao wa Ira uliopo katika jimbo la Kwara na kuzikwa Jumamosi. Lakini Ikpeba akiongea katika kipindi cha Monday Night Football kinachorushwa hewani na luninga ya Supersport aliweka sawa suala hilo kwa kusema kuwa hakuna chuki ya aina yoyote iliyojengwa na baadhi ya wachezaji juu ya Yekini katika kikosi cha mwaka 1994. Ikpeba ambaye amewahi kuichezea klabu ya AS Monaco aliendelea kufafanua kuwa mashindano ya kutafuta nafasi katika kikosi cha timu ya taifa ya nchi hiyo yanaweza kuwa yamechuliwa vibaya na mashabiki wa soka kupelekea kurusha tuhuma hizo. Mchezaji huyo wa zamani aliendelea kusema kwamba alikuwa sehemu ya kikosi cha mwaka 1994 na hakubaliani kuwa kulikuwa na kundi linalompinga mchezaji akitolewa mfano wa rekodi ya mabao 37 aliyofunga katika michezo 58 aliyochezea kikosi hicho mabao ambayo yametengenezwa na wachezaji wenzake aliocheza nao kipindi hicho. Ikpeba ambaye kwasasa ni mtangazaji wa Supersport alimsifu Yekini kwamba ni mmoja wa washambuliaji bora aliowahi kupata kucheza nao na ndio maana mpaka sasa hakuna mshambuliaji mwingine aliyefikia rekodi yake ya mabao aliyoweka.

No comments:

Post a Comment