Sunday, May 27, 2012

BARRY HATIHATI KUSHIRIKI EURO.



KIUNGO wa kimataifa wa Uingereza na klabu ya Manchester City, Gareth Barry anatarajiwa kufanyiwa vipimo kufuatia kuumia kiuno katika mchezo baina ya timu yake na Norway uliochezwa jijini Oslo. Barry ambaye alitolewa nje baada ya kuingia kama mchezaji wa akiba katika kipindi cha mapumziko ambapo tulishuhudia kikosi hicho kinachonolewa na Roy Hodgson kikipata ushindi wa bao 1-0 ukiwa ni ushindi wa kwanza katika ardhi ya Norway katika miaka 32 iliyopita. Kuumia kwa Barry itakuwa ni pigo kwa Hodgson ambaye sasa atalazimika kutafuta mbadala wa mchezaji huyo kabla ya Jumanne ambapo atataja kikosi chake cha mwisho kwa ajili ya michuano ya Ulaya. Kuna uwezekano mkubwa Hodgson akamchagua kiungo wa Liverpool Jordan Henderson ambaye ndiye aliziba nafasi ya Barry wakati akitolewa nje, kuziba kabisa pengo la mchezaji huyo katika kikosi cha mwisho cha timu hiyo kama akishindwa kupona kwa wakati.

No comments:

Post a Comment