Monday, May 21, 2012

RONALDO KUNG'ARA EURO 2012 - GULLIT.

Ruud Gullit.
MCHEZAJI nyota wa zamani wa kimatiafa wa Uholanzi, Ruud Gullit anadhani kuwa nyota wa Ureno Cristiano Ronaldo anaweza kung’aa katika michuano ya Ulaya kama atacheza katika kiwango ambacho amekuwa akicheza katika klabu yake. Ronaldo ambaye ana umri wa miaka 27 amefunga mabao 46 katika michezo 38 aliyoichezea timu yake ya Real Madrid na kuisadia timu hiyo kunyakuwa taji la Ligi Kuu nchini Hispania msimu huu. Gullit amesema kuwa mbali na Ronaldo kung’aa katika michuano hiyo pia wachezaji wa timu ya taifa ya Uholanzi Robin van Persie na Arjen Robben nao pia wanaweza kuonyesha kiwango cha juu baada ya kumaliza msimu wakiwa na mafanikio. Mchezaji huyo ambaye amewahi kuisaidia nchi yake kunyakuwa taji la Ulaya mwaka 1988 aliendelea kusema kuwa wachezaji hao wataingia katika michuano hiyo wakiwa na kiu ya mafanikio baada ya kushindwa kunyakuwa Kombe la Dunia mwaka 2010 wakifungwa katika hatua ya fainali hivyo hii itakuwa ni nafasi yao nyingine ya kuonyesha makali yao. Uholanzi inatarajiwa kuanza kampeni zake katika michuano ya Ulaya kwa kucheza dhidi ya Denmark June 9 mwaka huu wakati Ureno itakutana na Ujerumani katika mchezo wao ufunguzi wa kundi B.

No comments:

Post a Comment