Sunday, May 27, 2012

FABREGAS NJE WIKI MBILI.

KIUNGO wa kimataifa wa Hispania na klabu ya Barcelona, Cesc Fabregas anatarajiwa kukosa sehemu ya maandalizi ya timu yake ya taifa kwa ajili ya michuano ya Ulaya baada ya kuumia msuli wa paja ambao utamuweka nje ya uwanja kwa siku 10. Fabregas aliumia wakati akiingia kama mchezaji wa akiba wakati wa mchezo wa fainali ya Kombe la Mfalme baina ya Barcelona na Athletico Bilbao mchezo ambao Barcelona ilishinda mabao 3-0. Mchezaji huyo wa zamani wa Arsenal anatarajiwa kujumuishwa katika kikosi chamwisho cha wachezaji 23 wa timu ya taifa ya nchi hiyo kitakachotajwa leo ambacho kitakwenda nchini Poland na Ukraine mwezi ujao kutetea taji lao la Ulaya. Kocha wa Hispania Vicente del Bosque mara ya kwanza alishindwa kuwaita wachezaji wa Barcelona na Bilbao kutokana na mchezo wa kombe la Mfalme uliokuwa ukiwakabili na sasa anakabiliwa na michezo miwili ya kimataifa ya kirafiki kwa ajili ya kujipima nguvu kabla ya kuanza kampeni za kutetea taji lao dhidi ya Italia June 10 mwaka huu.

No comments:

Post a Comment