Wednesday, May 23, 2012

ARSENAL YAACHA SABA.

Emmanule Almunia.
KLABU ya Arsenal ya Uingereza inatarajia kuwaachia wachezaji wake saba ambao mikataba yao inaishia Juni 30 mwaka huu. Katika taarifa iliyotolewa katika mtandao wa klabu hiyo wachezaji ambao wataondoka ni pamoja na Manuel Almunia, George Brislen-Hall, Gavin Hoyte, Sean MacDermott, Rhys Murphy, James Campbell na Jeffrey Monakana. Kati ya wachezaji hao ni Almunia na Hoyte ndio waliofanikiwa kucheza katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo, ambapo Almunia ambaye ni golikipa amekichezea kikosi cha kwanza michezo 175 toka alipojiunga na klabu hiyo Julai mwaka 2004 akitokea klabu ya Celta Vigo. Taarifa hiyo iliyotumwa katika mtandao iliwashukuru wachezaji hao kwa mchango wao katika kipindi chote ambacho wamekuwepo klabuni hapo na wanawatakia kila kheri katika maisha yao ya soka huko watakapoenda.

No comments:

Post a Comment