Saturday, May 26, 2012

GERRARD AFURAHI KUPEWA UNAHODHA UINGEREZA.


 

KIUNGO wa kimataifa wa Uingereza, Steven Gerrard anatarajiwa kukiongoza kikosi cha timu ya taifa ya nchi hiyo katika michuano ya Ulaya inayotarajiwa kuanza mapema mwezi ujao akiwa kama nahodha. Gerrard amepewa unahodha wa timu hiyo ikiwa ni miezi mitatu imepita toka afikirie kwamba hataweza tena kukiongoza kikosi cha nchi yake baada ya aliyekuwa kocha wa timu hiyo Stuart Pearce kumpa unahodha kiungo wa Tottenham Hotspurs Scott Parker katika kipindi chake. Lakini ujio wa kocha mpya Roy Hodgson ambaye aliwahi pia kuwa kocha wa Liverpool umeonyesha kutimiza ndoto za Gerrard baada ya kukabidhiwa rasmi unahodha wa timu ya Uingereza kwa mara ya kwanza na anatarajia kukiongoza kikosi hicho kwenye mchezo dhidi ya Norway. Akihojiwa Gerrard amesema kuwa alisikitika kushindwa kukiongoza kikosi cha timu hiyo ambacho kilicheza na Uholanzi baada ya aliyekuwa kocha wa kipindi hicho Pearce kumwambia kwamba hawezi kuwa nahodha wa timu hiyo.

No comments:

Post a Comment