Nyimbo tamu aiseee ya long time but still rocking
Friday, March 30, 2012
Robbie williams and wife Ayda are expecting their first baby CONGRATULATION
hilo kisssssxxxxxx yummy
Mwanamziki mkongwe wa England kaanounce rasmi kuwa mke wake ayda anatarajia kujifungua mtoto hivi karibuni na he cant wait being called a daddy for the first time wooooow haya ndo maneno robbie mwenyewe akiiambia media
'Hey friendlies, I've been keeping a secret from you all. Me and Ayda are going to be a Mummy and Daddy this year!!!!!!!!
Je wajua viungo vya chakula vinavyosaidia kupunguza mwili?
1. Mdalasini
4. Pilipili Mtama(Black Pepper)
6. PiliPili Kichaa
Pilipili inauwezo wa kufanya mwili kudigest chakula haraka.
7.Tangawizi
Harufu ya mdalasini humfanya mtu asijisikie hamu ya kula, pia hudhibiti kiwango cha sukari kwenye damu hivyo kuzuia mkusanyiko wa mafuta mwilini. Ongeza mdalasini kwenye kawaha, chai, asali.
2.IlikiIliki ina chembechembe zinazozuia mkusanyiko wa mafuta kwenye mwili.Unaweza kuitumia Iliki kwenye chai, maziwa, kahawa.
3. Jeera ( Cumin)
Zamani Ugiriki walikua wanawapa wanariadha wao Jeera kabla ya mashindano ili wasisikie njaa kuepuka kuwapa chakula kabla ya mashindano na kuwajaza matumbo kabla ya michuano.Itumie Jeera kila unapojisikia njaa itakufanya ujihisi umeshiba. Mbali na hayo ina ladha nzuri na huleta harufu nzuri kinywani.
4. Pilipili Mtama(Black Pepper)
Ina uwezi wa kuua seli zenye mafuta mwilini.Pia inasaidia sana kupunguza kiungulia.
5. Manjano.
Manjano inasaidia sana kwenye digestion ya chakula. Pia inauwezo wa kuzuia cell kujikusanya na kutengeneza mafuta mwilini.
6. PiliPili Kichaa
Pilipili inauwezo wa kufanya mwili kudigest chakula haraka.
7.Tangawizi
Tangawizi huongeza joto mwilini, kwa hiyo kuharakisha metabolic processes mwilini.
Inawezekana ulikua unatumia tu, bila ya kujua kua viungo hivi vina manufaa mengine zaidi ya kuongeza ladha kwenye chakula. Niameanzaje sasa kuvitumia kwa fujo mie...xoxoxooo
TAARIFA MBALIMBALI KUTOKA TFF LEO.
LWIZA KUSIMAMIA EL MERREIKH, PLATINUM CL
Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limemteua Alfred Kisongole Lwiza kuwa Kamishna wa mechiya Ligi ya Mabingwa (CL) kati ya El Merreikh ya Sudan na FC Platinum ya Zimbabwe. Mechi hiyo ya marudiano ya raundi ya kwanza itachezwa Aprili 7 mwaka huu kwenye Uwanja wa El Merreikh jijini Khartoum, Sudan kuanzia saa 2 kamili usiku. Katika mechi ya kwanza iliyochezwa wikiendi hii jijini Harare timu hizo zilitoka sare ya mabao 2-2. El Merreikh ni moja ya timu ambazo CAF iliziingiza moja kwa moja katika raundi ya kwanza. FC Platinum iliingia raundi ya kwanza baada ya kuing’oa Green Mamba ya Swaziland katika raundi ya awali.
ZIMBABWE YAITAKA TWIGA STARS
Chama cha Mpira wa Miguu Zimbabwe (ZIFA) kimeomba mechi ya kirafiki kati ya timu yake ya Taifa ya wanawake na Twiga Stars. Mechi hiyo itakayochezwa kati ya Aprili 28 au 29 mwaka huu jijini Harare. Mechi hiyo ni sehemu ya maandalizi ya timu ya Zimbabwe kwa ajili ya kutafuta tiketi ya kucheza Fainali zaNane za Kombe la Afrika kwa Wanawake (AWC) zitakazofanyika Novemba mwaka huu nchini EquatorialGuinea. Twiga Stars ambayo iko kambini mkoani Pwani tangu Machi 25 mwaka huu chini ya Kocha Charles Boniface Mkwasa nayo inajiwinda kwa fainali hizo ambapo itacheza mechi ya kwanza Mei 26 mwaka huu jijini Addis Ababa dhidi ya Ethiopia. Zimbabwe yenyewe inacheza na Senegal. Machi 10 mwaka huu, Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara alizindua akaunti ya Twiga Stars kupitia Tigo Pesa kuichangia timu hiyo ili ishiriki vyema michuano ya AWC. Wachangiaji wa Twiga Stars wanatakiwa kutuma mchango wao kwenda namba 13389 ambapo kiwango cha juu kinachoweza kutumwa kwa muhamala (transaction) mmoja ni sh. 500,000. Katika uzinduzi huo, Waziri Dk. Mukangara alichangia sh. milioni moja.
MTIHANI WA MAWAKALA WA WACHEZAJI
Mtihani kwa ajili ya mawakala wa wachezaji wanaotambuliwa na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) utafanyika Machi 31 mwaka huu saa 4 kamili asubuhi ofisi za Shirikisho la Mpira wa MiguuTanzania (FIFA). Watu watatu wamejitokeza kufanya mtihani huo utakaokuwa na sehemu mbili. Sehemu ya kwanza ni maswali kutoka FIFA wakati nyingine ni kutoka TFF.
SIMBA, YANGA ZASAKA POINTI VPL
Yanga na Simba ni miongoni mwa timu nne zitakazokuwa viwanjani kesho (Machi 31 mwaka huu) kusaka pointi tatu za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) ambayo iko katika raundi ya 22. Uwanja wa Mkwakwani, jijini Tanga utakuwa mwenyeji wa mechi namba 148 kati ya Coastal Union na Yanga. Mechi hiyo itachezeshwa na mwamuzi Rashid Msangi wa Dodoma ambaye atasaidiwa na Rashid Lwena (Ruvuma) na Issa Malimali (Ruvuma). Mwamuzi Amon Paul wa Musoma ndiye atakayechezesha mechi namba 151 kati ya African Lyon na Simba itakayochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Viingilio kwenye mechi ya African Lyon na Simba ni sh. 3,000 kwa viti vya kijani na bluu, sh. 5,000 viti vya rangi ya chungwa, sh. 10,000 kwa VIP C na B wakati VIP A ni sh. 15,000. Aprili Mosi mwaka huu kutakuwa na mechi ya VPL kati ya Azam na Ruvu JKT itakayochezwa Uwanja wa Chamazi, Dar es Salaam. Kiingilio katika mechi hiyo kitakuwa sh. 1,000 kwa mzunguko na sh. 5,000 jukwaa kuu.

SENEGAL MGUU NJE MGUU NDANO OLIMPIKI.
SIMBA wa Teranga, Senegal watamenyana na Oman katika mechi maalum ya kuwania tiketi ya kucheza Olimpiki mwaka huu, London, mchezo utakaofanyika Aprili 23 mjini Coventry. Mechi hiyo itaamua timu ya mwisho ya kukamilisha idadi ya timu 16 za kucheza Olimpiki inayotarajiwa kuanza Julai 26 hadi Agosti 11, mwaka huu. Simba wa Teranga wamepata nafasi hiyo baada ya kushika nafasi ya nne katika michuano ya Afrika ya vijana chini ya umri wa miaka 23 iliyofanyika Morocco Desemba mwaka jana. Oman inayofundishwa na Mfaransa, Paul Le Guen walipata nafasi hiyo baada ya kuifunga Uzbekistan 2-0 Alhamisi katika mechi ya mwisho ya kuwania kufuzu kucheza fainali hizo kwa bara la Asia. Gabon, Morocco Misri ni wawakilishi wengine wa Afrika kwenye Olimpiki ya mwaka huu. Timu nyingine zilizofuzu ni mbali na wenyeji Uingereza, ni kwa upande wa bara ya Asia ni Korea Kusini, Japan, Falme za Kiarabu, huku Brazil na Uruguay ikiwakilisha Amerika Kusini, wakati Uswisi, Hispania na Belarus wakiwakilisha Ulaya na New Zealand wakiwakilisha OCEANIA. Wawakilishi wengine wawili watatoka Amerika Kaskazini, michuano yao inatarajiwa kumalizika Jumatatu ijayo.
MADRID KUFUNGUA ACADEMY CHINA.
VIGOGO wa Ulaya, Real Madrid wako mbioni kufungua shule ya soka nchini China mwakani, wakiungana na klabu ya Ligi Kuu ya China, Guangzhou Evergrande, taarifa ambayo imetolewa na mmiliki klabu hiyo ya China katika tovuti yake. Madrid, ambao ni mabingwa mara nyingi zaidi Ulaya, wakiwa wameshinda kombe hilo mara tisa, wako katika mpango wa kujitangaza zaidi na wameingia China, ambayo inavutia klabu nyingine kubwa Ulaya. Shule hiyo itakayokuwa kusini mwa jiji la Guangzhou, itakuwa na wachezaji wapatao 3,000 katika mwaka wa kwanza, watakaokuwa wakitumia vifaa na kufundishwa kwa ubora ule ule wa shule ya Real Madrid nchini Hispania. Kocha wa vijana wa klabu hiyo ya Hispania, Fernando Sanchez Cipitria ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Ufundi.
BERLUSCONI AKIRUDIA KITI CHAKE MILAN.
WAZIRI Mkuu wa zamani wa Italia Silvio Berlusconi amekalia rasmi kiti chake cha urais wa klabu ya AC Milan ya nchini humo baada ya kujiuzulu uongozi wan chi hiyo Novemba mwaka jana. Taarifa kutoka klabuni hapo imetangaza kuwa Bodi ya Wakurugenzi wa klabu hiyo ilimteua Berlusconi kama rais wa heshima wa klabu hiyo. Siku zote Berlusconi amekuwa akikaimu nafasi ya urais wa klabu hiyo, ingawa makamu wa rais Adriano Galliani amekuwa akiiendesha klabu hiyo kwa shughuli za kila siku. Kiongozi huyo wa zamani wa nchi hiyo ambaye alijiuzulu kutokana na matatizo ya kiuchumi yaliyoikumba Italia mwaka jana amewahi kuwa rais wa Milan kutoka mwaka 1986 mpaka 2004 na kurudia tena nafasi hiyo mwaka 2006 mpaka 2008. Katika hatua nyingine mshambuliaji wa klabu hiyo Antonio Cassano ameanza kufanya mazoezi na wachezaji wenzake kwa mara ya kwanza toka alipofanyiwa upasuaji mdogo wa moyo Novemba mwaka jana ingawa bado anahitaji kupona zaidi ili aweze kucheza na hata kuwa na muda wa kujiunga na kikosi hicho katika michuano ya Klabu Bingwa ya Ulaya.
MARADONA BLASTS 'COWARDS' AFTER WIFE ATTACK.
KOCHA wa klabu ya Al Wasl ya Muungano wa Falme za Kiarabu-UAE amewashambulia mashabiki wa huko na kuwaita waoga baada ya kulazimika kukimbilia jukwaani kumuokoa rafiki yake wa kike ambaye alikuwa akishambuliwa na mashabiki wenye hasira. Nguli huyo wa soka wa zamani kutoka Argentina alishuhudia timu yake hiyo ikipoteza mchezo dhidi ya Al Shabab kwa mabao 2-0 katika Ligi Kuu ya UAE wakati wake na marafiki wa kike wa wachezaji wakilazimika kuzindikizwa kutoka nje ya Uwanja wa Al Mamzar, Dubai. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na luninga moja maarfu nchini humo ya Gulf ilisema kuwa vurugu hizo zilianza wakati mshambuliaji wa Mbrazil wa Al Shabab aitwae Ciel ambaye alifunga mojawapo ya mabao ya timu yake mashabiki wa Al Wasl. Mashabiki wa Al Shabab nao wakajibu mapigo kwa kumgeukia rafiki yake wa kike Maradona na aitwae Veronica Ojeda na kuanza kumtupia maneno ya kumdhalilisha. Akihojiwa mara baada ya tukio Maradona amesema kuwa kitendo hicho kimemsononesha sana kwakuwa hakutegemea mashabiki hao wangekuwa waoga kiasi hadi kupelekea kuwashambulia wanawake badala ya kumshambulia yeye mwenyewe.
Thursday, March 29, 2012
Wednesday, March 28, 2012
wanasema age is nothing but a number eehh.....
Morgan Freeman
E’Dena Hines (mjukuu anaedaiwa kuwa na mahusiano na Morgan),katikati ni Myrna Colley-Lee (aliekuwa mke wa Morgan) na Morgan kabla ya talaka.
E’Dena Hines na Morgan "kwa lugha nyingine maharusi watarajiwa".... lol
Inasemekana muigizaji wa siku nyingi Morgan Freeman mwenye miaka 75 anatarajia kumuoa mjukuu wake wa kambo E’Dena Hines 30 (mjukuu wa aliekuwa mke wake wa kwanza Juanette Adair Bradshaw,kwa mtoto aliezaa kabla ya kuolewa na Morgan). Morgan baada ya kuachana na mkewe huyo alimuoa Myrna Colley-Lee mwaka 1984 ambae nae aliachana nae 2008 baada ya skendo za Morgan kua na mahusiano na E'Dena. By the way hii habari ni ya muda mrefu, sijui why wameirudisha mitandaoni kwa sasa. Au vikao vya harusi ndio vinaanza!!!??
Kama humjui Morgan Freeman unaweza kuangalia movies zake kama Along came the spider 2001, Bruce Almighty 2003, Nurse Betty 2000 . The guy is good in acting....ila hili swala la kuoa mjukuu wake hata kama si kwa mtoto wake wa kumzaa mhhhhhh...........
MANCHESTER UNITED ENJOY REFEREEING 'ADVANTAGE' - VIERA.
MCHEZAJI wa zamani wa kimataifa wa Ufaransa ambaye kwasasa ni mmoja wa maofisa wa klabu ya Manchester City, Patrick Viera amesema kuwa wapinzani wao katika mbio za ubingwa wa Ligi Kuu ya Uingereza Manchester United wanasaidiwa na makosa ya waamuzi. Kauli hiyo imekuja ikiwa ni siku mbili baada ya timu ya Fulham kukataliwa penati katika dakika za mwisho katika mchezo baina ya United na timu hiyo uliochezwa katika Uwanja wa Old Trafford ambapo wenyeji waliibuka na ushindi wa bao 1-0. Matokeo hayo yanaifanya United kukaa kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo wakiwa na alama tatu zaidi ya wapinzani wao City. Akihojiwa Viera amesema kuwa United wakati wanacheza nyumbani wanapata faida kama hizo ambazo timu zingine hazipati na sio United pekee hata ukicheza na Real Madrid, Barcelona au AC Milan matatizo kama hayo huwa yanatokea. Aliendelea kusema kuwa faida kama hizo huwa zinapata timu ambazo zimezoea kupata ushindi mara zote hivyo na wao wanahitaji kushinda michezo mingi zaidi ili waweze kupata faida kama hizo huko mbeleni. Wakiwa wamebakisha michezo nane, City wamejikuta wakiwa nyuma ya United kwa alama tatu lakini Viera ambaye amechukua nafasi kama Ofisa wa Maendeleo wa klabu hiyo baada ya kustaafu kucheza anaamini kuwa City wanastahili kuwa mabingwa.
SHEIKH KHALIFA WA UAE AMWAGA MINOTI KWA VIJANA WAKE.
RAIS wa Falme za Kiarabu-UAE Sheikh Khalifa bin Zayed ameipa timu ya taifa ya nchi hiyo ya vijana chini ya miaka 23 ambao wamefanikiwa kufuzu michuano ya Olimpiki inayotarajiwa kufanyika jijini London mwaka huu euro 100,000 kila mmoja. Timu hiyo imefanikiwa kukata tiketi ya kucheza michuano hiyo kwa mara ya kwanza katika historia ya mpira ya nchi hiyo kwa kuifunga Uzbekistan kwa mabao 3-2 mapema mwezi huu. Hayo ni mafanikio makubwa kabisa katika historia ya soka ya nchi hiyo yenye utajiri mkubwa wa mafuta toka timu ya wakubwa ya nchi hiyo ilipofanikiwa kukata tiketi ya kushiriki michuano ya Kombe la Dunia mwaka 1990 kwa mara ya kwanza. Sheikh Khalifa aliwapokea wachezaji wa timu hiyo pamoja na viongozi wao katika kasri lake la Dhiyafa lililopo Abu Dhabi mapema wiki hii kabla ya kuwakabidhi zawadi hiyo.
KOREA KUSINI KUJIPIMA NGUVU NA HISPANIA.
CHAMA cha Soka cha Korea Kusini-KFA kimetangaza mkakati wake wa kupambana na mabingwa wa dunia Hispania Mei 30 mwaka huu. Timu ya taifa ya Korea inajipanga kumaliza mzunguko wake wa mwisho wa mechi za kufuzu michuano ya Kombe la Dunia 2014 mwezi Juni mwaka huu hivyo mchezo huo utakuwa mahsusi kwa ajili ya maandalizi ya michezo hiyo. Korea ambao wanajulikana kwa jina la utani la Taeguk Warriors wako katika kundi A wakiwa na timu za Iran, Uzbekistan, Qatar na Lebanon ambapo wanatarajia kucheza mchezo wao wa mzunguko wa nne jijini Doha Juni 8 mwaka huu. Kwa upande wa Hispania wao watatumia mchezo huo kama maandalizi ya michuano ya Ulaya ambayo inatarajiwa kuchezwa Juni mwaka huu huko Poland na Ukraine ambapo mabingwa hao watetezi wa michuano hiyo wamepangwa kundi C wakiwa na timu za Italia, Jamhuri ya Ireland na Croatia.
HEART SPECIALIST: MUAMBA UNLIKELY TO RETURN.
BAADA ya moyo kushindwa kufanya kazi wakati wa mchezo wa Kombe la FA kati ya Bolton Wanderers na Tottenham Hotspurs katikati ya mwezi huu Fabrice Muamba hatarajiwi kucheza soka tena kwa mujibu wa daktari bingwa wa magonjwa ya moyo. Mkurugenzi mtabibu wa Mfuko wa Magonjwa ya Moyo Peter Weissberg amekiri kuwa itakuwa sio suala sahihi kwa mtu kumshauri mchezaji huyo wa zamani wa timu ya taifa ya Uingereza ya vijana chini ya miaka 21 kuendelea kucheza soka. Weissberg anaelewa kuwa suala la Muamba kucheza soka tena sio rahisi kwa sababu tatizo la kusimama kwa moyo wake kufanya kazi limechangiwa kwa kiasi kikubwa na na mazoezi anayofanya hivyo itakuwa sio busara mchezaji huyo kurejea uwanjani tena. Akihojiwa Weissberg amesema kuwa sio rahisi kusema kwasasa lakini anafikiri mchezaji atashauriwa kutocheza soka tena kwasababu tatizo hilo lililomkumba linachangiwa kwa kiasi kikubwa na mazoezi magumu anayofanya. Tatizo la moyo kwa wachezaji mpira limekuwa ni la kawaida kutokana na matukio mengi kuwa yanatokea katika miaka ya hivi karibuni wakiwemo wachezaji kama Ruben de la Red na Sergio Sanchez kupumzika kucheza kutokana na matatizo hayo wakati Marc Vivien Foe, Antonio Puerta na Dani Jargue wote walikufa kutokana na matatizo ya moyo.
Tuesday, March 27, 2012
MADRID, CHELSEA ZATENGENEZA MAZINGIRA MAZURI YA KUSONGA MBELE.
KLABU za Chelsea na Real Madrid jana usiku zimefanikiwa kushinda michezo yao ya kwanza ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na kujiweka kwenye mazingira mazuri ya kutinga Nusu Fainali. Salomon Kalou aliunganisha krosi ya Fernando Torres dakika ya 75, kuipatia Chelsea ushindi wa 1-0 dhidi ya Benfica jijini Lisbon, Ureno, huo ukiwa ushindi wa kwanza ugenini kwa timu hiyo kwenye mashindano hayo msimu huu. Nchini Cyprus, Karim Benzema alifunga bao la kichwa dakika ya 74 akimalizia krosi safi iliyopigwa na Kaka, huku Kaka nae akifunga bao la pili wakati Benzema alipoongeza lingine dakika ya 82 na kuihakikishia ushindi Real Madrid wa mabao 3-0 dhidi ya APOEL Nicosia. Michezo ya marudiano baina ya timu hizo itapigwa Aprili 4 mwaka huu ambapo Chelsea wataikaribisha Benfica katika Uwanja wa Stamford Bridge huku Madrid wakiwakaribisha APOEL katika Uwanja wa Santiago Bernabeu nchini Hispania. Michezo mingine ya kwanza ya robo fainali inatarajiwa kuendelea tena leo ambapo mabingwa watetezi wa michuano hiyo Barcelona watachuana na AC Milan huku Olympic Marseille wakiikaribisha Bayern Munich huko Ufaransa.
TAARIFA MBALIMBALI KUTOKA TFF LEO.
VITA VPL YAHAMIA MORO UNITED, VILLA
Timu za Moro United na Villa Squad ambazo ziko kwenye vita ya kukwepa kushuka daraja katika Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) zinapambana kesho (Machi 28 mwaka huu) kwenye moja kati ya mechi mbili za siku hiyo. Mechi hiyo namba 153 itachezwa kwenye Uwanja wa Chamazi, Dar es Salaam kuanzia saa 10 kamili. Moro United iko nafasi ya 11 ikiwa na pointi 18 wakati Villa Squad iko nafasi ya 14 kwa pointi zake 14. Viingilio katika mechi hiyo ni sh. 1,000 kwa mzunguko na sh. 5,000 kwa jukwaa kuu. Mwamuzi atakuwa Andrew Shamba akisaidiwa na Samson Kobe na Idd Mikongoti wote wa Dar es Salaam. Kamishna wa mechi hiyo atakuwa Arthur Mambeta wa Dar es Salaam wakati mtathmini wa waamuzi (referees assessor) ni Emmanuel Chaula kutoka mkoani Rukwa. Mechi nyingine ya Machi 28 mwaka huu itakayochezeshwa na mwamuzi Judith Gamba wa Arusha itakuwa kati ya Ruvu Shooting itakayoikaribisha Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Mabatini ulioko Mlandizi mkoani Pwani. Gamba katika mechi hiyo namba 150 atasaidiwa na Saada Tibabimale kutoka Mwanza na Hellen Mduma wa Dar es Salaam. Mwamuzi wa akiba ni Juma Safisha wa Pwani wakati Kamishna ni Hamis Kissiwa wa Dar es Salaam. Mechi za Machi 31 mwaka huu ni Coastal Union dhidi ya Yanga kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga, wakati Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam utakuwa mwenyeji wa mechi ya African Lyon na Simba.
RHINO, POLISI DAR KUANZA FAINALI FDL
Timu za Rhino Rangers ya Tabora na Polisi Dar es Salaam zitapambana Machi 31 mwaka huu katika moja ya mechi za ufunguzi wa fainali za Ligi Daraja la Kwanza zitakazochezwa Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro. Kila siku zitachezwa mechi mbili, moja ikianza saa 8 mchana wakati ya pili ni saa 10 jioni ambapo fainali hiyo itamalizika Aprili 22 mwaka huu kwa timu tatu za kwanza kupanda Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) msimu ujao- 2012/2013. Morogoro imepewa uenyeji baada ya kulipa sh. milioni 20.5 kati ya sh. milioni 25 zilizotakiwa. Sh. milioni 4.5 zilizobakia imekubaliana na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kuwa itazilipa moja kwa moja kwenye huduma zitakazotumiwa na wasimamizi wa fainali hizo. Mkoa mwingine ulioomba uenyeji ulikuwa Mbeya. Lakini wenyewe hadi Machi 26 mwaka huu ambayo ilikuwa siku ya mwisho kufanya malipo ulikuwa umeingiza kwenye akaunti ya TFF sh. milioni 15. Upangaji ratiba (draw) ulifanyika jana (Machi 26 mwaka huu) kwenye ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na kushuhudiwa na viongozi wa timu saba kati ya tisa zinazocheza fainali hizo. Mechi ya pili siku ya ufunguzi itakuwa kati ya Trans Camp na Mbeya City Council. Aprili Mosi ni Tanzania Prisons na Polisi Morogoro zitakazocheza mchana wakati jioni ni Mgambo Shooting na Mlale JKT. Aprili 2 mwaka huu ni Polisi Tabora vs Rhino Rangers (mchana) na Polisi Dar es Salaam vs Trans Camp (jioni). Aprili 3 mwaka huu ni Mbeya City Council vs Tanzania Prisons (mchana) na Polisi Morogoro vs Mgambo Shooting (jioni). Aprili 5 mwaka huu ni Polisi Tabora vs Mlale JKT (mchana) wakati jioni ni Rhino Rangers vs Trans Camp. Aprili 6 mwaka huu Polisi Dar es Salaam vs Mbeya City Council (mchana) wakati jioni ni Tanzania Prisons vs Mgambo Shooting. April 8 mwaka huu ni Mlale JKT vs Polisi Morogoro (mchana) wakati jioni itakuwa Polisi Tabora vs Polisi Dar es Salaam. Aprili 9 mwaka huu ni Mgambo Shooting vs Rhino Rangers (mchana) wakati jioni ni Trans Camp vs Tanzania Prisons. Aprili 11 mwaka huu ni Mbeya City Council vs Polisi Tabora (mchana) na Mlale JKT vs Rhino Rangers (jioni). Aprili 12 mwaka huu Polisi Dar es Salaam vs Mgambo Shooting (mchana) na Polisi Morogoro vs Trans Camp (jioni).
LIGI YA TAIFA KUANZA APRILI 22
Kamati ya Mashindano ya TFF iliyokutana Machi 24 mwaka huu imepitisha michuano ya Ligi ya Taifa Ngazi ya Taifa inayoshirikisha mabingwa wa mikoa ianze Aprili 22 mwaka huu kwenye vituo vitatu tofauti. Wakati Machi 26 mwaka huu ndiyo ilikuwa mwisho kwa vyama vya mikoa kuwasilisha TFF majina ya mabingwa wao, ni mikoa minne tu iliyomudu kufanya hivyo kwa mujibu wa kalenda ya matukio ya TFF. Mikoa hiyo na mabingwa wake kwenye mabano ni Kigoma (Kanembwa FC ya Kibondo), Ruvuma (Mighty Elephant ya Songea), Kilimanjaro (Forest FC ya Siha) na Dodoma (CDA ya Dodoma Mjini).Hivyo Kamati ya Mashindano imeongeza muda hadi Aprili 9 mwaka huu kwa mikoa ambayo haijawasilisha majina ya mabingwa wao iwe imefanya hivyo. Kwa itakayoshindwa ndani ya muda hiyo, mabingwa wao hawatapata fursa ya kucheza ligi hiyo. Kamati imetoa pongezi kwa mikoa hiyo minne kwa kuhakikisha imechezesha ligi yao kwa mujibu wa kalenda ya matukio ya TFF. Pia imepanga makundi matatu ya ligi hiyo. Kundi A lina mikoa ya Rukwa, Mbeya, Ruvuma, Iringa, Morogoro, Lindi na Mtwara. Kundi B lina mabingwa wa mikoa ya Kigoma, Tabora, Shinyanga, Mwanza, Mara, Kagera, Singida na Dodoma. Kundi C ni Dar 1, Dar 2, Dar 3, Pwani, Tanga, Kilimanjaro, Arusha na Manyara. TFF inakaribisha maombi ya uenyeji kwa kila kundi. Taarifa rasmi itatumwa kwa vyama mikoa kueleza masharti ya kutimiza kabla ya mkoa kupewa kituo cha ligi hiyo. Mshindi katika kila kundi na washindwa bora (best losers) wawili kutoka kwenye makundi yenye timu nane watapanda daraja msimu ujao kucheza Ligi Daraja la Kwanza (FDL). Pia timu zinatakiwa ziwe zimefanya usajili wa wachezaji kufikia Aprili 10 mwaka huu wakati Aprili 11-18 itakuwa ni kipindi cha kutangaza majina na pingamizi.
KOMBE LA FA KUANZA TENA MSIMU UJAO
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limerejesha tena mashindano ya Kombe la FA (TFF) kuanzia msimu ujao 2012/2013 ambapo bingwa wa michuano hiyo ataiwakilisha Tanzania katika michuano ya Kombe la Shirikisho. Timu zinazotakiwa kushiriki michuano hiyo itakayochezwa kwa mtindo wa mtoano ni zilizosajiliwa ambapo katika maombi yao ni lazima ziambatanishe nakala ya hati ya usajili wa klabu ambayo itatakiwa kuidhinishwa na chama cha mpira wa miguu cha wilaya. Ada ya fomu ya maombi ya kushiriki ni sh. 20,000 wakati ada ya mashindano ni sh. 200,000. Usajili wa wachezaji katika Kombe la FA ni ule ule mmoja wa kalenda ya usajili ya TFF ambapo unaanza Juni Mosi na kumalizika Septemba 10.

BECKHAM KUUZA MAGARI YAKE YA KIFAHARI.
Moja ya magari ya kifahari ya David Beckham. |
Hivi karibuni Beckham alionekana katika jiji la Los Angeles akitumia pikipiki katika matembezi yake maeneo mbalimbali ya mji huo.
ABIDAL KUPIGWA KISU.
BEKI wa Barcelona, Eric Abidal anatarajiwa kufanyiawa upasuaji wa kupandikiza ini katika hospitali moja nchini Barcelona. Taarifa zilizotolea na klabu hiy zinasema kwamba mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa amechangiwa ini hilo atalopandikizwa kutoka kwa rafiki yake wa karibu ambaye wamekuwa wote toka utotoni. Kulikuwa kuna wasiwasi kwamba Abidal asingecheza tena soka ya ushindani baada ya upasuaji kama huo mwaka jana, lakini Mfaransa huyo alipona na kurudi kazini akicheza soka safi katika ushindi wa 3-1 wa Barca dhidi ya Manchester United katika fainali ya Ligi ya Mabingwa kwenye Uwanja wa Wembley. Abidal pia hivi karibuni alisaini mkataba mpya na Barcelona ambao haujaweka wazi ni kwa muda gani mchezaji huyo ataitumikia klabu hiyo..
REAL MADRID, CHELSEA KIBARUANI ULAYA LEO.
MICHUANO ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya inaendelea tena leo ambapo viwanja viwili vitawaka moto katika michezo ya robo fainali ya michuano hiyo. Katika michezo ya leo timu ya APOEL Nicosia itakuwa na kibarua kigumu wakati itapoikaribisha timu ya Real Madrid katika wake wa nyumbani nchini Ugiriki huku wpinzani wao hao wakipewa nafasi kubwa ya kushinda mchezo huo. Kocha wa Madrid Jose Mourinho amewatahadharisha wachezaji wake kuwa mchezo huo hautakuwa rahisi hivyo wajizatiti na kucheza katika kiwango chao cha juu baada ya siku za hivi karibuni kuonekana wakilegalega katika Ligi Kuu nchini Hispania kwa kupoteza baadhi ya pointi. Mchezo mwingine ambao nao unatarajiwa kuwa mgumu utakuwa ni kati ya Benfica ya Ureno ambao wataikaribisha Chelsea katika uwanja wao wa nyumbani ambapo ushindi wataoupata katika mchezo huu wa kwanza utawaweka katika nafasi nzuri ya kusonga mbele. Chelsea itaingia uwanjani ikiwa na kumbukumbu nzuri ya kuitoa Napoli kwa ushindi wa kushangaza chini ya kocha wake Roberto Di Matteo ambaye toka alipoanza kuinoa klabu hiyo imeonekana kurudi kwenye kiwango kizuri licha ya kufungwa na Manchester City katika mchezo wa LIgi Kuu nchini Uingereza.
MUAMBA AIZINDUA FIFA.
Jiri Dvorak. |
HAVELANGE HALI TETE.
RAIS wa zamani wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), Joao Havelange ameingia katika wiki ya pili tangu alazwe katika hospitali ya Samaritano na yuko katika hali mbaya kwa sababu ya madhara yanayomsibu kwenye kifundo cha mguu wake wa kulia. Taarifa ya hospital ya Samaritano imesema juana kwamba babu huyo mwenye umri wa miaka 95 sasa, Havelange anatibiwa kwa dawa za antibiotics na afya kwa hakika si njema. Havelange alilazwa Machi 18 kutokabna na matatizo yake hiyo yanayosababisha kudhoofu kwa kiungo, ingawa anapumua bila msaada wa mashine. Alistaafu kwenye Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki mwaka jana, kwa sababu za kiafya. Havelange alikuwa rais wa FIFA tangu 1974-98.
Monday, March 26, 2012
Malavidavi si kwenye Movie tu hadi kwenye real life..!!
Inasemekana movie stars Robert Pattinson na Kristen Stewart wana uhusiano wa kimapenzi nje ya movie wanayoigiza pamoja ya The Twilight. Lakini waigizaji hao hawako tayari kuuzungumzia uhusiano wao.
Robert na Christen wakiwa wamekaa seat za nyuma ya gari wakijificha kuepuka mapaparazzi.
Kama bado hujaona series hizo za Twilight jaribu kutafuta copy yako ujionee, ziko nne tu mpaka sasa.
Sunday, March 25, 2012
Saturday, March 24, 2012
Mashindano ya Mister Africa in People's Friendship University of Russia
Mshiriki kutoka Gabona alikuja kwa style hii
Guinea Ecuatorial waliwakilishwa hivi, by the way huyu jamaa alikua
na pozi za "kisharobaro" mnoo hapo jukwaani
Visiwa vya Shelisheli (Seychelles) nao walikuwepo, hivi ndivyo walivyowakilishwa
Jamaa kutoka Kisiwa cha Sao Tome, huyu kaka anajua kuipamba nchi yake aisee
Kuna waliokuja kwa mwendo huu, shurti mtu kabebwa,hapana chezea Ivory Coast
Mshiriki kutoka Nigeria, Tuliimbishwa "Umofia Kwenu" ukumbi mzima
Kwa mara ya kwanza kwa historia ya Umoja wa nchi za Africa chuo kikuu cha Urafiki zamani "Lumumba" Umeendesha mashindano ya kumtafuta "Mr.Africa".Too bad Video Camera haikuwepo kuwaletea matukio yalivyokua. Mwisho wa siku mshindi wa kwanza alitoka Nigeria, wa pili kutoka Ivory Coast na wa tatu Sao Tome.
Subscribe to:
Posts (Atom)