Friday, May 25, 2012

BECKHAM KUTUNUKIWA.


 

SHIRIKISHO la Soka barani Ulaya-UEFA linatarajia kumtunukia nishani nahodha wa zamani wa timu ya taifa ya Uingereza, David Beckham kama mchezaji aliyecheza michezo zaidi ya 100 ya kimataifa katika mchezo baina ya Uingereza na Ubelgiji unaotarajiwa kuchezwa June 2 mwaka huu. Chama cha Soka nchini humo-FA kimetoa taarifa kwamba Beckham mwenye umri wa miaka 37 ambaye amecheza michezo 115 katika timu ya taifa ya Uingereza kabla ya kustaafu mwaka 2009 atatunukiwa nishani katika muda wa mapumziko wakati wa mchezo huo. Mbali ya Beckham nishani hiyo pia watapewa mshambuliaji nyota wa zamani ambaye aliiwezesha Uingereza kunyakuwa Kombe la Dunia mwaka 1966, Bobby Charlton ambaye alicheza michezo 106 na golikipa mstaafu wa timu hiyo Peter Shilton ambaye anashikilia rekodi ya kucheza michezo mingi zaidi akiwa na michezo 125. Sherehe hizo za kuwatunuku wachezaji ambao wamecheza mechi nyingi katika timu zao za taifa zitazinduliwa na rais UEFA Michel Platin.

No comments:

Post a Comment