Sunday, May 27, 2012

HULK AIBEBA BRAZIL.


 

MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Brazil na klabu ya Porto Hulk ameonyesha dalili kwamba anataka kuwemo katika kikosi cha timu ya taifa ya nchi hiyo ambacho kitashiriki michuano ya Olimpiki jijini London. Hulk ambaye ana umri wa miaka 25 alionyesha kiwango cha juu katika mchezo ambao Brazil iliifunga Denmark mabao 3-1 ambapo alifunga mabao mawili katika kipindi cha kwanza huku akisababisha lingine la tatu mchezaji wa Denmark Niki Zimling kujifunga mwenyewe. Mchezaji huyo ambaye anapigania nafasi tatu katika kikosi hicho kwa wachezaji ambao wamezidi umri wa miaka 23 anaamini kuwa kiwango chake kinaweza kumshawishi kocha wa timu hiyo Mano Menezes kumjumuisha katika kikosi kitachoshiriki michuano hiyo. Brazil imepangwa kundi moja na timu za Misri, Belarus na New Zealand kwa ajili ya michuano ya Olimpiki 2012 ambao Menezes anatarajiwa kutangaza kikosi kamili Julai 6.

No comments:

Post a Comment