Saturday, May 26, 2012

HENRY MCHEZAJI ANAYELAMBA MKWANJA MREFU MAREKANI.

MSHAMBULIAJI wa klabu ya New York Red Bulls, Thierry Henry ndiye mchezaji anayelipwa fedha nyingi zaidi katika Ligi Kuu nchini Marekani-MLS akimzidi kiungo nyota wa klabu ya Los Angeles Galaxy David Beckham. Henry mwenye umri wa miaka 34 analipwa kiasi cha dola milioni 5.6 kwa mwaka kwenye mkataba aliosaini na klabu hiyo mwaka huu akimzidi Beckham ambaye ndiye aliyekuwa akilipwa zaidi. Katika mkataba mpya Beckham aliosaini na klabu hiyo mapema mwaka huu alikubali kupunfguziwa mshahara wake pamoja na baadhi ya marupurupu aliokuwa akpewa. Namba mbili katika orodha ya wachezaji wanaolipwa zaidi katika ligi hiyo inashikiliwa na Rafa Marguez kutoka Mexico ambaye nae anacheza katika klabu ya Red Bull akikunja kitita cha dola milioni 4.6. Beckham ambaye wakati akitua nchini Marekani mwaka 2007 ndio alikuwa mchezaji anayelipwa zaidi katika ligi hiyo akikunja kitita cha dola milioni 6.5 kwa mwaka hivi sasa amedondoka mpaka nafasi ya tatu akiwa analipwa kiasi cha dola milioni nne kwa mwaka.

No comments:

Post a Comment