Friday, May 25, 2012

MFUMO HAWK-EYE KUFANYIWA MAJARIBIO WEMBLEY.


 

SHIRIKISHO la soka Duniani-FIFA limesema kuwa linatarajia kufanya majaribio ya mfumo wa teknologia ya kompyuta katika mstari wa goli unaoitwa Hawk-Eye wakati wa mchezo wa kimataifa wa kirafiki baina ya timu ya taifa ya Uingereza na Ubelgiji mchezo ambao utafanyika katika Uwanja wa Wembley jijini London. Kampuni ya kujitegemea ya EMPA na wawakilishi kutoka FIFA ndio wanatarajiwa kuufuatilia mfumo huo wakati ukifanyiwa majaribio katika mchezo huo ingawa hautatumiwa na waamuzi wa mchezo huo utakaochezwa June 2 mwaka huu. Mfumo wa Hawk-Eye pia ulifanyiwa majaribio katika fainali ya Kombe la Ligi ndogo nchini Uingereza kati ya timu ya Eastleigh na AFC Totton uliofanyika Aprili mwaka huu. Mfumo mwingine ambao unaitwa GoalRef wenyewe ulifanyiwa majaribio katika michezo miwili ya Ligi Kuu nchini Denmark mwezi huu, ambapo taarifa kamili juu ya mfumo upi ambao utatumika itaamuliwa katika kikao cha Kamati ya Kimataifa ya Soka-IFBA itakayokutana Julai mwaka huu.

No comments:

Post a Comment