Thursday, May 3, 2012

LA LIGA NI NGUMU KULIKO LIGI ZINGINE - MOURINHO.

KOCHA wa klabu ya Real Madrid, Jose Mourinho anaamini kuwa ushindi wa taji la Ligi Kuu nchini Hispania maarufu kama La Liga ulikuwa mgumu kuliko mataji mengine sita aliyoshinda akiwa kocha wa vilabu nchini Ureno, Uingereza, Italia na Hispania. Madrid ilifanikiwa kuifunga Athletico Bilbao kwa mabao 3-0 na kuwawezesha kubakisha pengo la alama saba dhidi ya mahasimu wao Barcelona huku wakiwa wamebakiwa na michezo miwili mkononi. Mourinho anakuwa kocha wa kwanza kushinda taji la ligi katika nchi nne tofauti kufuatiwa kushinda mataji mawili ya Ligi Kuu nchini Ureno wakati akifundisha klabu ya Porto, mawili katika Ligi Kuu nchini Uingereza wakati akifundisha Chelsea na mawili mengine nchini Italia wakati akiwa na klabu ya Inter Milan. Akihojiwa mara baada ya mchezo huo Mourinho ambaye ana umri wa miaka 49 amesema kuwa ushindani ulikuwa mkubwa sana kwani hadi muda huo hakuna aliyekuwa akiwapa nafasi ya wao kuwa mabingwa msimu huu.

No comments:

Post a Comment