Thursday, May 17, 2012

TEVEZ AKATAA KUOMBA MSAMAHA KWA FERGIE.

MSHAMBULIAJI wa Manchester City Carlos Tevez amemnanga kocha wa Manchester United Sir Alex Ferguson kwamba anajifanya kama rais wa Uingereza. Kauli ya Tevez imekuja kufuatia kubeba bango liliandikwa “RIP Fergie” wakati timu yake hiyo ikisherehekea kunyakuwa ubingwa wa Ligi Kuu ya nchi hiyo katika mitaa ya jiji la Manchester ingawa baadae City waliomba msamaha kwa tukio hilo lakini Tevez aligoma kuomba msamaha. Akihojiwa kuhusu tukio hilo Tevez amesema kuwa kwa anavyoona yeye ni kwamba Ferguson ni kama rais wa Uingereza kwani mara nyingi amekuwa akisema maneno yasiyo ya kiungwana juu yake(Tevez) lakini hakuwahi kumwambia amwombe msamaha. Tevez alikuwa ameshikilia bango hilo alilopewa na mashabiki wa City ikiwa ni kama kumjibu kocha huyo kwa kauli yake aliyoitoa kabla ya mechi baina ya timu hizo mwaka 2009. Kabla ya mchezo huo Ferguson aliulizwa kama United inaweza kuwa chini City katika siku za mbeleni na kocha huyo alijibu kuwa haiwezi kutokea wakati akiwa hai, kauli ambayo iliwakera sana mashabiki wa City.

No comments:

Post a Comment