Saturday, May 19, 2012

RAFAEL AITWA BRAZIL KUZIBA PENGO LA ALVES.


 

BEKI wa kimataifa wa Brazil na klabu ya Manchester United, Rafael ameitwa katika kikosi cha timu ya taifa ya nchi hiyo kuziba pengo la beki wa Barcelona Daniel Alves ambaye ni majeruhi. Shirikisho la Soka la nchi hiyo-CBF lilitangaza kuwa Rafael amejumuishwa katika kikosi hicho kinachonolewa na kocha Mano Menezes kwa ajili ya michezo minne ya kimataifa ya kirafiki ambayo itafanyika baadae mwezi huu na mwezi ujao. Kujiunga kwake na timu hiyo anatimiza idadi ya wachezaji 18 katika kikosi cha vijana chini ya miaka 23 ambao wanahitajika kwa ajili ya michuano ya Olimpiki itakayofanyika jiji London michuano ambayo Brazil imepania kuondoka na medali ya dhahabu. Alves alivunjika mfupa wa mguu wake wa kulia wakati wa mazoezi na timu yake ya Barcelona Jumatano ambapo anatarajiwa kuwa nje ya uwanja kwa muda wa wiki nane.

No comments:

Post a Comment