Monday, May 14, 2012

MAN CITY BADO WANA SAFARI NDEFU KUTUFIKIA - FERGUSON.

AKIWAPONGEZA Manchester City kunyakuwa taji la Ligi Kuu nchini Uingereza, kocha wa klabu ya Manchester United Sir Alex Ferguson aliwaonya wapinzani wao hao kuwa bado wana safari ndefu kufikia mafanikio waliokuwa nayo wao. Ferguson aliendelea kusema kuwa City ambao wamenyakuwa taji kwa mara ya kwanza baada ya miaka 44 wana kazi kubwa ili kufikia historia ambazo United imeziweka. Kocha huyo ambaye ana miaka 70 amesema kuwa itawachukua City miaka 100 ili kufikia mafanikio ambayo United imeweka katika soka la nchi hiyo. Ferguson aliwapongeza wachezaji wake kwa mchango wao waliotoa msimu mzima na pia aliwapongeza majirani zao City kwa ubingwa waliopata.

No comments:

Post a Comment