Wednesday, May 2, 2012

HENRY KUKAA NJE MWEZI.

MSHAMBULIAJI wa klabu ya New York Red Bulls ya Marekani, Thierry Henry anatarajiwa kukaa nje ya uwanja kwa muda wa wiki tatu au nne kutokana na majeraha ya misuli ya mguu wake wa kulia. Henry alipata majeraha hayo baada ya kufunga bao pekee katika ushindi wa bao 1-0 iliyopata timu yake dhidi ya New England Jumamosi iliyopita na kumuwezesha kufukisha mabao tisa na kuongoza orodha ya wafungaji katika Ligi Kuu nchini humo. Taarifa za klabu hiyo zinasema kuwa mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa alifanyiwa vipimo Jumatatu na kuonyesha kwamba majeraha aliyoyapata hayakuwa makubwa kama ilivyofikirika mara ya kwanza na mchezaji huyo atakaa nje kwa muda wa mwezi mmoja tu. Lakini majeraha hayo yatamuweka nje mchezaji huyo wakati wa mchezo wa Jumamosi baina ya timu yake na mabingwa watetezi wa ligi hiyo Los Angeles Galaxy ambayo anaichezea kiungo nyota wa Uingereza, David Beckham.

No comments:

Post a Comment