Tuesday, May 15, 2012

HAZARD ATHIBITISHA KUTUA UINGEREZA.


 

KIUNGO mshambuliaji wa klabu ya Lille ya Ufaransa Eden Hazard amethibitisha kuwa anatarajia kucheza jijini Manchester msimu ujao, lakini amekataa kuweka wazi ni klabu gani haswa ataichezea katika jijini hilo kati ya Manchester City au Manchester United. Kauli hiyo ya mchezaji huyo ameitoa wakati wa sherehe za utoaji tuzo ambapo alipewa tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa Ligi Kuu nchini Ufaransa maarufu kama Ligue 1 kwa mara ya pili mfululizo. Hazard ambaye ana umri wa miaka 21 ameripotiwa na vyombo vya habari nchini Ufaransa kunyemelewa na vilabu hivyo viwili nchini Uingereza kwa kipindi kirefu sasa. Lille imeweka dau la dola milioni 51 kwa mchezaji huyo wa kimataifa wa Ubelgiji kwa timu yoyote ambayo itahitaji saini yake.

No comments:

Post a Comment