Wednesday, May 16, 2012

FIFA YAVITILIA MASHAKA VIWANJA SITA VYA KOMBE LA DUNIA, BRAZIL.

SHIRIKISHO la Soka la Dunia-FIFA linaamini kuwa viwanja sita kati ya 12 ambavyo vitatumika kwa ajili ya michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2014 havitakuwa tayari kwa muda uliopangwa. Gazeti la Folha ambalo lilitizama tathmini iliyofanywa na maofisa wa FIFA kuhusiana na ujenzi wa viwanja vipya pamoja na vile vinavyofanyiwa ukarabati ilionyesha viwanja vya Manaus, Cuiaba, Porto Alegre, Curitiba na Sao Paulo hatari zake ni za kati. Lakini tatizo kubwa liko katika uwanja uliopo Kaskazini-Mashariki mwa jiji la Natal kwa sababu muda wake wa matengenezo na mahali ulipofikia hakutahitajika kutokea tatizo lolote kwani ikitokea hivyo ni wazi hautakamilika kwa wakati. Taarifa hiyo pia inaonyesha kuwa ikiwa imebakia miaka miwili kabla ya kuanza kwa michuano ya Kombe la Dunia matengenezo ya viwanja 12 vitakavyotumika kwa ajili ya michuano hiyo imefikia asilimia 34.4.

No comments:

Post a Comment