Tuesday, March 20, 2012

Ukistaajabu ya musa......

  Natasha Moraes de Andrade (miaka 12) ni mkazi wa  Rio De Janeiro, Brazil. Binti huyu ana nywele  zenye urefu wa futi 5 na nchi 3, ila sasa ametangaza kuzikata  kwa dau la 3500£ ambayo ni sawa na 7.5 m tsh. 

  Kwa wiki natumia kopo zima la shampoo, masaa manne kuziosha na nusu saa kuzichana. 
Mtoto huyu haishi maisha ya kawaida kama ya watoto wengine wa umri wake kwa maana nywele zinamzuia kucheza, kufanya mazoezi. Mama yake aitwaye  Moreas de Andrade amesema imefika muda inabidi nywele hizo zikatwe maana zimezidi kuongeza bajeti kwenye familia, ambayo familia inashindwa kuimudu.kwa mwaka wanatumia   400£ ambayo ni sawa na 85,0000 tsh kuzihudumia nywele hizo.       
  Natasha anatarajia kuzitumia pesa zake hizo atakazozipata baada ya kupata mteja kufanyia ukarabati chumba chake.
Haya mama kata nywele watutengenezee maweaving na mawig tuvae.dau lake mmeliona eeh, no wonder hizo brazilian hair tunauziwa bei...lol

No comments:

Post a Comment