Saturday, February 11, 2012

Rest in Peace Whitney Houston


  Mwanamuziki na Muigizaji Whitney Houston amekutwa amekufa kwenye chumba cha Hoteli  huko Los Angeles Marekani jana jumamosi. Whitney alikua in Los Angeles na marafiki na familia yake kwa ajili ya Grammy Awards ambazo zinafanyika leo usiku.
    Sababu ya kifo chake hakijajulikana na polisi wanaendelea na uchunguzi wao.
   
 Whitney atakumbukwa sana kwa nyimbo zake kama I will always love you, I learned from the best, own my own,  My love is your love na nyingine nyingi. Pia kwa movies zake  ikiwemo The Bodyguard iliyotokea kupendwa sana.
  
  Whitney amefariki akiwa na miaka 48. Aliwahi kua mke wa Bobby Brown ambae wamefanikiwa kupata mtoto mmoja. Katika kipindi cha uhai wake amewahi kujihusisha na matumizi ya madawa ya kulevya na Bangi ambayo kwa kiasi kikubwa yalichangia sana kupotea kwake kwenye fani ya Muziki. Mwaka 2009 alirudi tena kwenye muziki, na wimbo wake wa I Look To You. Rest in Peace Whitney
                                           
                                            I look To You- Whitney Houston
       
                          

No comments:

Post a Comment