Thursday, June 28, 2012

UINGEREZA HAIWEZI KUSHINDA KOMBE LA DUNIA - SHEARER.

NAHODHA wa zamani wa kimataifa wa Uingereza, Alan Shearer anaamini kuwa nchi hiyo haina nafasi ya kunyakuwa taji la michuano ya Kombe la Dunia litakalofanyika nchini Brazil mwaka 2014 kutokana na kiwango cha chini walichokionyesha katika michuano ya Ulaya. Kikosi cha nchi hiyo ambacho kinanolewa na kocha Roy Hodgson kiling’olewa katika robo fainali michuano ya Ulaya kwa changamoto ya mikwaju ya penati na timu ya taifa ya Italia. Akihojiwa Shearer amesema kuwa hamlaumu Hodgson kwa kutolewa kwa timu hiyo kwenye michuano hiyo lakini haamini kama itafika siku moja nchi itaondoka katika michuano mikubwa wakiwa na taji. Nyota huyo wa zamani aliendelea kusema kuwa itakuwa si jambo jema kama wakijipa moyo kwamba wanaweza kushinda kombe la dunia katika kipindi cha miaka miwili inayokuja wakati kiukweli hawataweza mpaka hapo jitihada za makusudi zitakapofanyika kwa timu hiyo ili iweze kucheza soka la kiushindani zaidi. Shearer amesema kuwa wasibweteke na suala kwamba Ligi ya Kuu ya nchi hiyo ndiyo bora kuliko zote duniani kwani ligi hiyo imejaa wachezaji wa kigeni, hivyo ni wakati umefika kuanza kubadilisha mfumo wa ufundishaji kuanzia timu za vijana za nchi hiyo ili kuendana na mfumo wa kisasa wa soka.

No comments:

Post a Comment