Friday, June 22, 2012

NIZAR, YONDAN WAANZA MAZOEZI JANGWANI.

Kelvin Yondan akipasha katika Uwanja wa Kaunda leo asubuhi. (Picha na Bin Zubery)
KLABU ya Soka ya Yanga imeanza mazoezi rasmi kwa ajili ya maandalizi ya kutetea ubingwa wao wa michuano ya Kagame pamoja na kuondoa machungu waliyopata msimu uliopita baada ya kufungwa na watani wao Simba mabao 5-0. Katika mazoezi hayo wachezaji wawili ambao wamesajiliwa msimu huu Nizar Khalfan na Kevin Yondan walikuwa kivutio kikubwa katika mizoezi hayo ambayo yalihudhuriwa na mamia ya mashabiki wa klabu hiyo kwenye Uwanja wa Kaunda. Khalfan alitua katika klabu hiyo akitokea klabu ya Vancouver Whitecaps ya nchini Canada wakati Yondani yeye ametokea klabu ya Simba ambapo usajili wake ulileta utata baada ya madai kuwa na mkataba na klabu yake ya zamani. Katika kuhakikisha inatetea ubingwa wa Kagame Yanga pia imewasajili mshambuliaji Said Bahanuzi kutoka Mtibwa, Frank Domayo kutoka JKT Ruvu na golikipa wa zamani wa Simba Ally Mustapha-Bathez. Yanga imeanza mazoezi chini ya kocha msaidizi wa klabu hiyo Fred Minziro wakati mazungumzo ya kumchukua Marcio Maximo kama kocha mkuu yakiwa bado yanaendelea.

No comments:

Post a Comment