Wednesday, June 20, 2012

RATIBA YA TIMU ZITAKAZOFUZU KUSHIRIKI AFCON KUPANGWA JULAI 5.



SHEREHE rasmi za upangaji wa ratiba ya timu zitakazofuzu michuano ya Mataifa ya Afrika 2013 zinatarajiwa kufanyika katika ukumbi wa Tanz Café jijini Johannesburg, Afrika ya Kusini Julai 5 mwaka huu. Nchi 14 ambazo zimefanikiwa kuvuka mzunguko wa kwanza wa kufuzu michuano hiyo zinatarajiwa kupambana na timu 16 ambazo zilishiriki michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika mapema mwaka huu ambapo ambapo timu 15 zitachujwa na kubakia 15 ambazo zitaungana na mwenyeji Afrika Kusini kwenye fainali hizo za mwaka kesho. Timu ambazo zimeingia katika mzunguko wa pili ni pamoja na Msumbiji, Zimbabwe, jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo-DRC, Ethiopia, Togo, Malawi, Uganda, Cameroon, Nigeria, Sierra Leone, Liberia, Cape Verde na Algeria. Misri na Afrika ya Kati-CAR zinatarajiwa kucheza mchezo wao marudiano jijini Bangui June 30 mwaka huu na mshindi atajumuishwa katika timu ambao zimetajwa hapo juu, CAR katika mchezo wa kwanza walifanikiwa kuifunga Misri mabao 3-2 jijini Alexandria wiki iliyopita.

No comments:

Post a Comment