Thursday, April 5, 2012

OLYMPIAKOS YATWAA UBINGWA WA UGIRIKI.

KLABU ya Olympiakos ya Ugiriki imefanikiwa kunyakuwa taji lake la 39 la Ligi Kuu ya nchi hiyo baada ya kupewa ushindi katika mchezo wake waliocheza March 18 mwaka huu baada ya mashabiki kufanya vurugu. Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka la nchi hiyo iliipa ushindi Olympiakos na kuwanyang’anya pointi tatu mahasimu wao timu ya Panathinaikos baada ya mashabiki wa timu hiyo kuanzisha vurugu katika Uwanja wa Olimpiki uliopo jijini Athens. Kwa maamuzi yaliyotolewa na kamati hiyo, Olympiakos imefikisha alama 67 kati ya michezo minne iliyobakia huku ikiwa imebakiza michezo mitatu wakati nafasi ya pili inashikiliwa na Panathinaikos akiwa na alama 57. Olympiakos pia imefuzu kucheza fainali ya Kombe la Ligi baada ya kufanikiwa kuifunga timu ya OFI ambapo sasa watakutana na timu ya Atromitos katika mchezo wa fainali mwezi ujao.

No comments:

Post a Comment