Sunday, April 22, 2012

KILL ME PLEASE: PART ONE

KATIKA MAISHA KUNA WATU WANAVIPAJI LAKINI HAWAJUI WAPI PAKUANZIA ILI WATOKE  KATIKA PEPESA PEPESA MACHO YANGU KWENYE MAKUNDI FULANI FULANI KATIKA FACEBOOK NILIKUTANA NA WADADA WENYE UWEZO WA KUWEZA KUTUNGA STORY ZAO WENYEWE  NA ZINASISIMUA HASWAA. BLOG YA NYUMBANI KWETU ITAKUA INAKULETEA STORY MBALI BALI KILA SIKU YA JUMAPILI KAMA UNAPENDA STORY KAMA ZA KINA SHIGONGO BASI HAPA UTAPATA UHONDO WA AINA YAKE LEO TUTAANZA NA STORY INAITWA KILL ME PLEASE NA MTUNZI NI NYEMO DAVID YEYE ANAUWEZO WA KUTUNGA FILAMU KALI KALI KUHUSIANA NA JAMII INAYOTUZUNGUKA HAYA PATA MAUTAMU.COM ( spare the grammatical errors)

KILL ME PLEASE: PART ONE

Nakushangaa unavyotaka kumuua huyo mtoto, ni mdogo sana na hana hatia kama unavyofikilia , kwa nini usiniue mimi badala yake! but plz usisahau sometime unaweza kumuua mtu anayekupenda kuliko unavyofikiria wewe, and i want to conferse to u that i love u! and am very happy to die while am in love with u....Olga aliyasema maneno hayo huku sura yake ikiwa imejawa na woga uliochanganyika na mapenzi ya dhati kwa jambazi hilo , je kwann Olga alilazimika kusema hayo plz fuatilia story hii inayokujia kwa hisan kubwa ya NYEmo Daaaavid.......
Olga, olga, olgaaaaaaaaaaaaaaaaaa eeeeeeeeeeeeeh hebu njoo bwana yaani husikiii ninavyokuita hivi wewe mtoto mbona unaniletea ujeuri siku hizi? Mama Olga anamuita bintiye mbaye kwa muda huo yuko chumbani anajifanyia home work zake , olga ni msichana wa miaka 16 na ametoka katika familia ya kimasikini mama samahani nilikuwa namalizia homework zangu, vp unasemaje mom,?mama samahani nilikuwa namalizia homework zangu, vp unasemaje mom,? Ok Olga naomba kesho uchelewe kdg kwenda shule ukae na mdogo wako miye nataka niende kwenye biashara zangu, mama ake Olga alikuwa anajishughulisha na uuzaji wa mboga ya kisamvu alichokuwa akienda kukichuma katika mashamba ya watu , Mama Olga alizoea kila siku asubuhi na mapema kumbeba mwanae ambaye alikuwa na mwaka mmoja na nusu kisha kwenda kwa marafiki zake waliokuwa na mashamba jirani, mama Olga aliwasaidia kidogo kazi , kisha nao kama kumpa asante walimruhusu kuchuma kisamvu ambacho alikuwa akienda kukitembeza katika manyumba ya watu na pesa alizozipata zilimsaidia katika kujikwamua na maisha magumu yaliyokuwa yakiwakabili hapo nyumbani......

Baba yake Olga alishawakimbia siku nyingi baada ya kuona maisha yamekuwa magumu pale nyumbani akaenda mkoa mwingine kuanza maisha mapya huko, kwa hiyo aliwaachia familia yake maisha yasiyokuwa hata na matumaini, lkn pamoja na hayo yote olga hakukata tamaa kwenye kujituma ! alisoma kwa bidii zote shida za pale nyumbani hazikumfanya alegeze uzi alijitahidi sana kwa kuona kuwa may be kwa kusoma kwake Mungu angekuja kuyageuza maisha yao hapoo baadae..... Olga alipoingia darasa la saba maisha yalizidi kuwazidia , na kuwa magumu at the same time Olga alitakiwa awe na vifaa vya shuleni kitu ambacho kilimuongezea mama yake gharama ,Olga alionekana kumuonea huruma sanamamake but hata hivyo angefanyaje? ihali yeye bado ni teneeger hakuwa hata na idea maisha ya nje yanaendaje kitu alichokiamini yeye ni shule na ndo maana alionyesha bidii zake zote! Olga alifanikiwa kufanya mtihani wa darasa la saba ambapo baadae majibu yalikuja na kuonyesha kuwa alikuwa miongoni mwa wasichana wachache hapo shuleni kwao waliochaguliwa kujiunga na elimu ya secondari, habari hizo zilileta mchanganyiko wa furaha na huzuni kwani hawakuelewa wangepata wapi pesa za kununua vifaa vya shule Wakiwa ktk kutafakari, mama Mayasa ambaye alikuwa ni best friend wa mama ya Olga alikuja na Idea kuwa kwann mama Olga asijaribu kupika pombe za kienyeji na kuwauuzia watu! maana hizo atleast angeweza kupata kipato cha kumnunulia bintiye vfaa vya shule, Idea hiyo ilipokelewa vzr na mama Olga kwa msaada mkubwa wa rafikiye mama Mayasa walianza kujiandaa kwa ajili ya kupika pombe hiyo kwanza walikoka moto mkali wa makuni , kisha wakatumbukiza maji ktk pipa kubwa na unga wakaanza kuyachemsha, huo mchanganyiko ulichemka kwa siku nzima, then jioni kama saa kumi na mbili wakayaipua mamchanganyiko hayo ili kuyapooza ndo wachanganyie na mchanganyiko mwingine hadi next day inakuwa pombe tayari, sasa walisaidiana na kuyaipua then wakagawanyisha katika mapipa mengine mawili ili upoe na then wakawa wanajaribu kupooza mara kwa mara , sasa ktk kupooza mdogo wa Olga alikuwa akipita pita katika kucheza na kwa bahati mbaya wazazi wake walijisahau na kufanya mambo mengine kwa bahati mbaya mtoto alikorofisha pipa moja na ule mchanganyiko wote ulimwagika na kumwagikia mtoto! tahamaki mama olga alijitahidi kumbeba mwanae na kumkimbiza hospital lkn kwa bahati mbaya madaktari walishindwa kuokoa maisha ya mtoto kwani alikuwa amebabuka mwili mzima kwa hiyo mtoto alipoteza maisha!Msiba wa mdogo wa Olga uliwaumiza sana watu, asubuhi na mapema kila mtu alikuwa akielekea kwenye msiba mama ya Olga alilia sana kwa kumkosa mwanae Olga naye alilia sana na alijilaumu kwa yote hayo yalitokea kwa sababu yake alimuhurumia sana mama yake kwa kupoteza mtoto ilimradi tu amsaidie olga aende shule, watu walikuja na kutoa pole nyingi kwa wafiwa , mama alizihifadhi hipo pole zote na baada ya msiba kwisha alizitumia pesa hizo ili kununua vfaa vya mwanae na hivyo ndivyo Olga alipoanza kidato cha kwanza kwa masikitiko makubwa moyoni alifikiria yaani mdogo wangu amejitoa sadaka ili tu nifanikiwe hakika nitajitahidi kwa kadri ya uwezo wangu ili nije kuyaenzi maisha ya mdogo wangu

Olga alifanikiwa kwenda shule na kuanza kidato cha kwanza huku akiwa na matarajio ya kujiendeleza ,na alijitahidi sana katika masomo yake hadi akaanza kuwashangaza walimu wake na mamake aliendelea na biashara yake ya kuuza mboga biashara ya pombe hakuitamani tena kwani ilimsababishia akampoteza mtoto wake aliyempenda sana , but biashara yake haikuwa nzuri tena kwani pesa alizokuwa anazipata ni kwa ajili ya kula tu so maisha yalianza kumuelemea sana hata hivyo jambo la kumshukuru mungu alikuwa peke yake tu kwani binti yake alikuwa ameenda shule so tumbo la mtu mmoja halikumpa shida sana Bahati mbaya ilianza tena olga alianza kukosa vifaa vya shule na kama mnavyojua hakuna hata mtu wa kumpiga jeki na hali hiiyo ikaanza kumfanya akate tamaa ya maisha, mwalimu Kipepe ambaye alikuwa ni mwalimu wake wa jiografia aliiugundua hali hiyo mara moja akaanza kutafuta mbinu za kumpata binti wa wawatu , kwanza alianza kwa kumpatia vijizawadi vya hapa na pale Olga hakuwa na wasiwasi kwani aliamini mwl alikuwa akimsaidia kwa nia njema kabisa na one day mwalim alimwambia olga kuwa Binti usiwe na wasiwasi nimeshapokea ada yako mama yako alishanitumia so we endelea vzr na shule wala usiwaze habari ya ada kumbe alikuwa anamdanganya hakuna ada iliyotolewa wala nini
TO BE CONTINUE..........

 
 
 
.
 

No comments:

Post a Comment