Wednesday, April 18, 2012

GUARDIOLA, DI MATTEO WAKIRI NGOMA BADO NZITO.

KOCHA wa Barcelona Pep Guardiola na Roberto Di Matteo wa Chelsea wamekubali kuwa nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya bado iko wazi baada ya mabingwa watetezi wa michuano Barcelona kufungwa na Chelsea bao 1-0 katika mchezo wa kwanza uliochezwa katika Uwanja wa Stamford Bridge jana. Guardiola amesema kuwa alitegemea mchezo wenye upinzani mkubwa kutoka kwa Chelsea na pia mchezo mwingine mgumu watakapokutana katika Uwanja wa Nou Camp wiki ijayo baada ya timu hiyo kupoteza mchezo wa kwanza. Kikosi cha Guardiola kilifanikiwa kutengeneza nafasi za kufunga 24 katika mchezo huo ingawa kocha huyo hakutegemea hilo, ingawa alisikitika kwamba hawakuzitumia nafasi hizo inavyostahili. Naye Di Matteo amesema kuwa alitizama mkanda wakati timu hiyo ilipocheza na AC Milan pamoja na mchezo dhidi ya Real Madrid ambapo Barcelona walicheza mchezo unaofanana kwa staili ya kipekee. Kocha huyo aliendelea kusema kusema kuwa ilibidi wafanye kazi ya ziada kuziba mianya ambayo wapinzani wao wanaweza kuitumia kupitisha mpira na kwa hilo walifanikiwa ingawa alikiri kuwa hadhani kama wataweza kuwazuia watapokwenda Camp Nou.

No comments:

Post a Comment