Monday, April 16, 2012

HATMA YA TEKNOLOGIA YA MSTARI WA GOLI KUJULIKANA JULAI.

SHIRIKISHO la Soka Duniani-FIFA limetangaza kuwa teknolojia ya kompyuta katika mstari wa goli inatarajiwa kuwa tayari kutumika mara baada ya majaribio ya mwisho ,kufanyika. Chama cha Mpira cha Kimataifa-IFAB, ambacho ndio hutunga sheria soka ndio kinafanyia majaribio ya pili teknologia hiyo kuangalia kama itafanikiwa. Mjadala wa kuingiza teknologia hiyo katika mchezo wa soka umeibuka tena baada ya mchezaji wa Chelsea, Juan Mata kufunga bao ambalo lilileta utata na kuisaidia timu hiyo kuingia fainali ya Kombe la Chama cha Soka nchini Uingereza-FA dhidi ya Tottenham jana. Picha za video zinaonyesha kuwa mwamuzi wa mchezo huo Martin Atkinson hakuwa sahihi kuwapa bao Chelsea kwa mpira hakuwa umevuka mstari wa goli. FIFA inatarajiwa kutoa uamuzi wa kutumia au kutotumia teknologia ya kompyuta katika mstari wa goli Julai 2 mwaka huu.

No comments:

Post a Comment