FAINALI ya michuano ya Ulaya ambayo timu ya taifa ya Hispania imefanikiwa kutetea ubingwa wake imevunja rekodi ya ujumbe mfupi wa mashabiki uliotumwa duniani kote ndani ya sekunde moja katika mtandao wa kijamii wa twitter. Fainali hiyo iliyochezwa Jumapili ambapo Hispania ilishinda mabao 4-0 dhidi ya Italia jumla ya watu milioni 16.5 walikuwa wakituma ujumbe katika mtandao huo, na watu 15,358 katika muda wa sekunde moja walituma ujumbe katika mtandao huo wakati bao la nne lilifungwa katika mchezo huo. Msemaji wa kampuni hiyo ambayo ndio inaendesha mtandao huo Andrew Fitzgerald amesema kuwa walikuwa wakipokea taarifa jinsi mashabiki walivyokuwa wakifuatilia michuano hiyo hatu kwa hatua. Fetzgerard aliendelea kusema kuwa mashabiki wa soka walikuwa wakituma ujumbe katika twitter wakitaja timu wanazozifuatilia na maoni yao kuhusu michezo iliyokuwa ikichezwa kuanzia hatua ya makundi, mtoano mpaka fainali. Mtandao wa kijamii wa twitter huwa unaruhusu watu waliojiunga kuweza kutuma ujumbe mfupi au picha ambapo unakadiriwa kuwa na watumiaji zaidi ya milioni 140 ambapo katika idadi hiyo wengi zaidi ni kutoka Marekani.
Tuesday, July 3, 2012
EURO 2012: TWITTER 15,358 ZIMETUMWA NDANI YA SEKUNDE MOJA WAKATI BAO LA JUAN MATA LIKITINGA WAVUNI.
FAINALI ya michuano ya Ulaya ambayo timu ya taifa ya Hispania imefanikiwa kutetea ubingwa wake imevunja rekodi ya ujumbe mfupi wa mashabiki uliotumwa duniani kote ndani ya sekunde moja katika mtandao wa kijamii wa twitter. Fainali hiyo iliyochezwa Jumapili ambapo Hispania ilishinda mabao 4-0 dhidi ya Italia jumla ya watu milioni 16.5 walikuwa wakituma ujumbe katika mtandao huo, na watu 15,358 katika muda wa sekunde moja walituma ujumbe katika mtandao huo wakati bao la nne lilifungwa katika mchezo huo. Msemaji wa kampuni hiyo ambayo ndio inaendesha mtandao huo Andrew Fitzgerald amesema kuwa walikuwa wakipokea taarifa jinsi mashabiki walivyokuwa wakifuatilia michuano hiyo hatu kwa hatua. Fetzgerard aliendelea kusema kuwa mashabiki wa soka walikuwa wakituma ujumbe katika twitter wakitaja timu wanazozifuatilia na maoni yao kuhusu michezo iliyokuwa ikichezwa kuanzia hatua ya makundi, mtoano mpaka fainali. Mtandao wa kijamii wa twitter huwa unaruhusu watu waliojiunga kuweza kutuma ujumbe mfupi au picha ambapo unakadiriwa kuwa na watumiaji zaidi ya milioni 140 ambapo katika idadi hiyo wengi zaidi ni kutoka Marekani.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment