Thursday, May 3, 2012

MUAMBA AWASHUKURU MASHABIKI.

KIUNGO wa klabu ya Bolton Wanderers Fabrice Muamba alirejea katika klabu yake hiyo jana na kuwapungia mashabiki waliojitokeza huku machozi yakimtoka ikiwa zimepita wiki saba toka mchezaji huyo alipoanguka na kuzimia uwanjani hapo. Muamba alitambulishwa kuwepo uwanjani hapo kabla ya mchezo wa Ligi Kuu ya nchini Uingereza baina ya timu hiyo na Tottenham Hotspurs ambayo ndiyo aliyokuwa akicheza nayo katika Kombe la FA wakati akianguka na kuzimia Machi 17 mwaka huu. Mchezaji huyo ambaye alionekana kuwa na afya njema alikuwa akifuta machoi mara kwa mara wakati akiwapungia mashabiki waliojitokeza katika Uwanja Reebok na kusema kwamba anatamani kama angekuwa anaweza kucheza siku hiyo. Moyo wa Muamba ulisimama kwa dakika 78 mara baada ya kunguaka lakini msaada wa haraka huduma ya ya kwanza aliopata pamoja na daktari bingwa wa magonjwa hayo ambaye alikuwa uwanjani hapo kama mshabiki walisaidia kuokoa maisha ya mchezaji huyo kijana.

No comments:

Post a Comment