Thursday, May 24, 2012

MTUKUTU BARTON AFUNGIWA MECHI 12.

NAHODHA wa QPR, Joey Barton amefungiwa mechi 12 na Chama cha Soka England kwa vurugu alizofanya kwenye mechi dhidi ya Manchester City katika siku ya mwisho ya msimu huu wa Ligi Kuu. Barton ameongezewa adhabu ya mechi nane katika mechi nne za awali sambamba na kutozwa faini ya pauni 75,000. Aligombana na Sergio Aguero na Vincent Kompany, lakini baada ya kupewa kadi nyekundu akamuanzishia na Carlos Tevez, na baadaye akawazingua marefa. Pamoja na hayo hajaadhibiwa kwa kwa kumsukumia kichwa Kompany, Tume Kanuni imesema katika taarifa kwa kitendo alichomfanyia Sergio Aguero anastahili adhabu hiyo.

No comments:

Post a Comment