Thursday, May 24, 2012

TFF YAICHOMOLEA MISRI MCHEZO WA KIRAFIKI.

Wachezaji wa Taifa Stars wakiwa mazoezini katika Uwanja wa Karume, Dar es Salaam.
SHIRIKISHO la Soka nchini-TFF limekataa ombi la Shirikisho la Soka la Misri la kuomba mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya timu ya taifa ya nchi hiyo maarufu kama Pharaohs ambao ulikuwa uchezwe Mei 28 mwaka huu. Misri waliandika barua TFF kuomba kucheza na Taifa Stars katika mchezo wa kirafiki ambao wangeugharamia wao kwa kila kitu lakini shirikisho hilo lilikataa kutokana na ufinyu wa muda unaowakabili katika ratiba yao. Akihojiwa Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura alithitisha shirikisho hilo kupata mwaliko kutoka Misri lakini kutokana na ufinyu wa muda katika ratiba yao walishindwa kukubali ombi hilo la kucheza na Pharaohs. Taifa Stars hata hivyo itacheza na Malawi katika mchezo wa kirafiki unaotarajiwa kuchezwa mwishoni mwa wiki hii kabla ya kuifuata Ivory Coast katika mchezo wa kwanza wa kufuzu michuano ya Kombe la Dunia 2014.

No comments:

Post a Comment