Wednesday, May 23, 2012

MOURINHO AJITIA KITANZI MPAKA 2016 MADRID.

KOCHA wa klabu ya Real Madrid, Jose Mourinho amekubali kuongeza mkataba wa miaka miwili na klabu hiyo utakaomuwezesha kuwepo mpaka mwishoni mwa msimu wa 2015-2016. Mourinho mwenye umri wa miaka 49 raia wa Ureno alikiongoza kikosi cha timu hiyo kunyakuwa taji la Ligi Kuu nchini Hispania baada ya miaka minne ya kulikosa kombe hilo. Timu hiyo chini ya uongozi wake imefanikiwa kuvunja rekodi ya mabao msimu huu wakiwa wameshinda mabao 121 na pia kuweka rekodi ya pointi 100 walizokusanya msimu mzima. Kabla ya kuinoa Madrid Mourinho pia amewahi kuzifundisha klabu za Inter Milan, Chelsea na FC Porto.

No comments:

Post a Comment