Thursday, May 17, 2012

CITY YAVUNJA BENKI KUMNYAKUWA IBRAHIMOVIC.

MANCHESTER City imetenga dau la paundi milioni 25 kwa ajili ya mshambuliaji wa AC Milan, Zlatan Ibrahimovic huku meneja wa timu hiyo Roberto Mancini akimuahidi mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Sweden mshahara wa paundi 300,000 kwa wiki. Kiasi hichi atacholipwa kitamfanya awe mchezaji anayelipwa mshahara mkubwa zaidi katika Ligi Kuu ya Uingereza, akimpiku kiungo wa City, Yaya Toure anayelipwa pauni250,000 kwa wiki. Ibrahimovic mwenyewe ambaye ana umri wa miaka 30 ameomba muda kufikiria suala hilo kabla ya kuamua kuweka saini kuichezea klabu hiyo tajiri nchini Uingereza. Hii ni mara ya pili kwa Mancini kujaribu kumsajili mshambuliaji huyo wa zamani wa Barcelona, Juventus na Inter Milan atue Eithad na safari hii anatarajia kufanikiwa. Mancini alimsajili Ibrahimovic wakati akiwa Inter Milan kwa pauni Milioni 22 mwaka 2006.

No comments:

Post a Comment