Sunday, April 15, 2012

PELE AITABIRIA SANTOS KUFANYA MAAJABU SIKU ZA USONI.

NGULI wa soka wa zamani wa Brazil, Pele ameeleza kuwa na imani na klabu yake ya zamani ya Santos kung’ara zaidi siku za usoni bada ya kuhudhuria hafla ya chakula cha usiku kwa ajili ya kusherekea miaka 100 toka kuanzishwa kwa klabu hiyo. Pele mwenye umri wa miaka 71 aliwasili katika sherehe hiyo kwa helikopta akiwa amebeba Kombe la Klabu Bingwa la Amrika Kusini maarufu kama Copa Libertadores na kupokewa na mashabiki wapatao 15,000 waliokuwepo wakati akitua katika hafla hiyo. Akizungumza katika hafla hiyo Pele alielezea kufurahishwa kwake kuwepo hapo na kukutana na marafiki wa zamani ingawa alisikitika kwamba sio wote waliokuwepo kwasababu ya kutangulia mbele haki. Pele pia alishukuru wachezaji wenzake ambao alicheza nao kipindi hicho wakati alipokuwa mchezaji wa klabu hiyo kwani bila wao asingepata mafanikio aliyopata akiwa na klabu hiyo. Mshambuliaji huyo nyota wa zamani anachukuliwa kama mchezaji bora aliyewahi kutokea katika klabu hiyo akiwa amefunga mabao zaidi ya 500 katika kipindi cha miaka 18 aliyoitumikia klabu hiyo.

No comments:

Post a Comment