Sunday, April 15, 2012

MESSI EQUALS RONALDO RECORD.

MSHAMBULIAJI wa Barcelona, Lionel Messi amefikia rekodi ya mshambuliaji wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo ya kufikisha mabao 41 kwa msimu mmoja baada ya kufanikiwa kufunga mabao mawili na kuiwezesha tmu yake kushinda mabao 2-1 dhidi ya Levante katika mchezo wa Ligi Kuu nchini Hispania maarufu kama La Liga. Levante ambao ndio waliotangulia kupata bao dakika ya 23 kwa njia ya penati iliyopigwa na Jose Barkero baada ya beki wa Barcelona Sergio Busquests kumfanyia madhambi katika eneo la hatari ingawa bao hilo halikudumu sana baada ya Messi kusawazisha dakika chache baadae. Messi alifunga bao la pili kwa mkwaju wa penalti dakika ya 72 na kuipa Barcelona ushindi wa 2-1 na kumfikia Ronaldo, ambaye aliweka rekodi hiyo kwa bao la dakika ya 74 la kichwa katika ushindi wa Real Madrid wa 3-1 dhidi ya Sporting Gijon. Madrid imeendelea kuongoza La Liga kwa tofauti ya pointi nne dhidi ya mabingwa watetezi mara tatu, Barcelona kabla ya mechi baina ya timu hizo, maarufu kama El Clasico wiki ijayo, ambayo itatoa picha ya mbio za ubingwa msimu huu zikiwa zimebaki mechi nne ligi kufikia tamati.

No comments:

Post a Comment