Wednesday, May 2, 2012
MARADONA KUTIMKA AL WASL.
MENEJA wa klabu ya Al Wasl ya Umoja wa Falme za Kiarabu-UAE amesema kuwa ana asilimia 50 ya kuondoka klabuni hapo baada ya mgogoro wake na uongozi wa klabu hiyo ambayo ilimuahidi kumpa fungu la wachezaji wa kiwango cha juu katika kipindi alipotua klabuni hapo. Nguli wa kimataifa wa Argentina ambaye alijiunga na Al Wasl Mei mwaka jana kwa mkataba wa miaka miwili alitishia kuiacha klabu hiyo kama uongozi utashindwa kumtimizia ahadi zake kama walivyomuahidi. Mapema wiki hii viongozi wa klabu hiyo walijibu vitisho vya Maradona kwa kudai kuwa wanatafuta mbadala wa kocha huyo kama akiamua kuikacha klabu hiyo huku Marcello Lippi na Gianfranco Zola wakihusishwa kufanya mazungumzo na klabu hiyo. Akihojiwa kuhusiana na sula hilo maradona amesema kuwa kama hatapewa fungu la kununua wachezaji ambao wataweza kuleta ushindani basi ana nafasi kubwa ya kujiuzulu wadhfa huo.
No comments:
Post a Comment