Wednesday, May 2, 2012
CITY YAZISOGELEA REAL MADRID NA BARCELONA KATIKA VILABU VINAVYOTOA MISHAHARA MINONO DUNIANI.
KLABU ya Manchester City inakamata nafasi ya tatu duniani katika orodha ya vilabu vinavyolipa mshahara mikubwa kwa mujibu wa utafiti mpya uliofanyika hivi karibuni. Orodha hiyo inatokana na mishahara mikubwa wanayowalipa wachezaji wake akiwemo kiungo wa klabu hiyo Yaya Toure ambaye anachukua kiasi cha paundi 86,000 kwa wiki kiasi ambacho kwa mwaka kinafikia paundi milioni 4.5 kiwango ambacho kinazidiwa na klabu ya ya Real Madrid na Barcelona pekee ambao ndio wanaongoza katika orodha hiyo. Utafiti huo ambao ulichapishwa katika mtandao unaonyesha kuwa klabu ya Chelsea mishahara kwa wachezaji wake imepanda na kwasasa wako chini ya City wakishika nafasi ya nne katika orodha hiyo. Manchester United wako katika nafasi ya 11 ambapo mchezaji anayepewa mshahara wa juu kabisa anapokea kiasi cha paundi milioni tatu kwa mwaka. City imeshangaza kupanda kwa haraka katika orodha hiyo toka Sheikh Mansour alipoinunua timu hiyo mwaka 2008 ambapo klabu hiyo ilikuwa ikishika nafasi ya 86 ambapo wakati utafiti huu ulipochapishwa tena mwaka 2010 klabu hiyo ilichupa mpaka nafasi ya 11. Sasa klabu hiyo iko nyuma ya vilabu vikubwa barani Ulaya na kuonyesha haja yao ya kuwa na wasiwasi juu ya sheria mpya ya matumizi ya fedha katika vilabu iliyotolewa na Shirikisho la Soka barani Ulaya-UEFA.
No comments:
Post a Comment