Tuesday, May 22, 2012

FIFA KUUNDA KAMATI MAALUMU KUSHUGHULIKIA UFISADI.


 

SUALA la ufisadi katika mchezo wa soka ndio linatarajiwa kuwa ajenda kubwa katika Mkutano Mkuu wa shirikisho la Soka Dunia ambao utakutanisha wajumbe wake wapatao 208 ambapo pia tunaweza kushuhudia mwanamke wa kwanza kteuliwa kuwa mjumbe wa kamati ya utendaji wa shirikisgho hilo. Katika mkutano huo FIFA inatarajiwa kuteua kamati huru kushughulikia tuhuma za ufisadi ambazo zimeuandama mchezo wa soka katika kipindi cha hivi karibuni ikiwemo suala la uapangaji matokeo katika baadhi ya michezo. Shirikisho hilo pia linatarajiwa kumtangaza mwanamke ambaye atapewa wadhifa wa ujumbe wa kamati ya utendaji wadhifa ambao ataushikilia kwa mwaka mmoja kabla ya uchaguzi mwingine. Kamati huru ya kushughulikia suala la ufisadi itakuwa na mamlaka ya kuchunguza tuhuma za rushwa zilizolikumba shirikisho hilo kipindi cha nyuma pamoja na kukagua hesabu za mwaka za shirikisho hilo. Majina ya wajumbe hao yamependekezwa na mpelelezi wa zamani wa Umoja wa Mataifa, Mark Pieth ambaye alichaguliwa na FIFA kuwa mshauri wa mambo kupambana na ufisadi.

No comments:

Post a Comment