MSHAMBULIAJI nyota wa kimataifa wa Ivory Coast, Didier Drogba amewaambia wachezaji wenzake wa timu ya Chelsea kwamba ataondoka katika klabu hiyo kwakuwa hapendi kubakia klabuni hapo kama mchezaji wa akiba. Drogba mwenye umri wa miaka 34 ambaye alifunga bao la kusawazisha dhidi ya Bayern Munich katika dakika za majeruhi na baadae kupiga mkwaju wa penati ambao uliipa ushindi wa kwanza katika historia ya klabu hiyo wa Kombe la Klabu Bingwa Ulaya Jumamosi iliyopita aliwapa taarifa hizo wachezaji wenzake huku machozi yakimtoka. Drogba alikaririwa akisema kuwa alishawahi kuwapa taarifa ya kuondoka wachezaji wenzake miaka mitatu iliyopita lakini hilo haikusaidia kumuweka katika wakati mgumu kama alipowapa taarifa hizo wachezaji wenzake wakati wanarejea Uingereza wakitokea Ujerumani na kombe lao la ubingwa. Mchezaji huyo alijiunga na mabingwa hao wa Ulaya mwaka 2004 akitokea klabu ya Olympique Marseille ya Ufaransa ambapo sasa anahusishwa kutaka kuhamia klabu ya Shanghai Shenhua ya nchini China.
Tuesday, May 22, 2012
DROGBA AWAAGA WACHEZAJI WENZAKE.

No comments:
Post a Comment