Tuesday, May 8, 2012

EURO 2012: LOEW APINGA KUSUSIA MECHI ZA UKRAINE.

KOCHA wa timu ya taifa ya Ujerumani, Joachim Loew amepinga wazo la kususia michuano ya Kombe la Ulaya itakayofanyika Ukraine kufuatia nchi hiyo kumuweka lupango Waziri Mkuu wake wa zamani Yulia Tymoshenko. Waziri mkuu huyo ambaye anatumikia kifungo cha miaka saba jela baada ya kukutwa na hatia ya kutumia vibaya madaraka yuko katika mgomo wa kula kutokana na kulalamika kutotendewa haki gerezani humo. Viongozi mashuhuri katika Umoja wa Ulaya na wengine walikuwa wakizungumzia suala la kususia michezo ambayo itachezwa Ukraine wakati wa mashindano hayo yanayotarajiwa kufanyika mwezi ujao. Akihojiwa na vyombo vya habari jana, Loew amesema kuwa yuko pamoja na Tysmoshenko ambaye anadai haki zake za msingi lakini kususia michezo itakayochezwa Ukraine hilo haoni kama lina maana. Ukraine na Poland ndio wenyeji wa michuano ya Kombe la Ulaya linalotarajiwa kuanza kutimua vumbi June 8 hadi Julai 1 mwaka huu.

No comments:

Post a Comment