Tuesday, May 15, 2012

ARSHAVIN KUIONGOZA URUSI EURO 2012.


 


KOCHA wa tmu ya taifa ya Russia Dick Advocaat amemteua Andrei Arshavin kuwa nahodha wa timu hiyo itakayoshiriki katika michuano ya Ulaya inayotarajiwa kuanza mapema mwezi ujao huko Ukraine na Poland. Advocaat ambaye ni raia wa Uholanzi atakifundisha kikosi hicho katika michuano hiyo ya Ulaya na baada ya hapo atarejea kuifundisha klabu ya PSV Eindhoven. Arshavin ameonyesha kurejesha makali yake miezi michache iliyopita baada ya kujiunga na klabu ya Zenit kwa mkopo akitokea Arsenal ya Uingereza na kuisaidia klabu hiyo kushinda kombe la Ligi Kuu ya Russia huku yeye akifunga mabao muhimu. Uamuzi wa kurejea nchini kwake umeonekana kumsaidia kujihakikishia namba katika timu ya taifa baada ya miaka mitatu isiyokuwa na mafanikio alipokuwa Arsenal. Russia imepangwa kundi moja na wenyeji Poland, Jamhuri ya Czech na mabingwa wa kombe hilo mwaka 2004 Ugiriki katika kundi A ambalo hata hivyo ndio linaonekana rahisi zaidi katika michuano hiyo.

No comments:

Post a Comment