Tuesday, May 15, 2012

ARSENAL YAMPA VAN PERSIE OFA YA MSHAHARA WA PAUNDI 130,000 KWA WIKI.


 

KLABU ya Arsenal inatarajia kuweka rekodi ya kulipa mshahara mnono zaidi wa paundi milioni saba kwa mwaka kwa ajili ya kumbakisha mshambuliaji wake nyota Robin van Persie. Meneja wa klabu hiyo Arsene Wenger, Ofisa Mkuu Ivan Gazidis na Van Persie mwenyewe wanatarajiwa kukutana kesho katika kikao kizito kujadili mkataba mpya wa mshambuliaji huyo nyota. Van Persie ambaye kwasasa analipwa kiasi cha paundi 70,000 kwa wiki anatarajiwa kuwa akilipwa mshahara wa paundi 130,000 kwa wiki katika mkataba wa miaka mitatu atakaopewa akiwazidi waliokuwa wachezaji nyota wa klabu hiyo Thierry Henry na Cesc Fabregas. Lakini pamoja na mchezaji huyo kuonyesha nia ya kubaki katika klabu hiyo yenye maskani yake Kaskazini mwa jiji la London bado anahitaji kuona ni timu gani zingine zikimuhitaji kabla ya kusaini mktaba huo mpya.

No comments:

Post a Comment