Thursday, April 5, 2012

PATO NJE MSIMU MZIMA.

DAKTARI wa klabu ya AC Milan Jean-Pierre Meersseman amethibitisha kuwa mshambuliaji Alexandre Pato atakuwa nje ya uwanja kwa msimu uliobakia baada ya kupata maumivu ya misuli. Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Brazil alikuwa amerejea katika kikosi hicho kilichocheza mchezo wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Barcelona baada ya kukaa nje kwa muda lakini alilazimika kutoka nje ya uwanjani baada ya dakika 14 alizocheza toka alipotoka benchi. Klabu hiyo inahofia mchezaji huyo kupata majeraha ya muda mrefu hivyo Meersseman ameona ni bora kumpumzisha mchezaji huyo kwa msimu uliobakia ili apone kabisa tayari kwa msimu ujao. Pato amecheza michezo 11 tu katika Ligi Kuu nchini Italia akiwa na timu hiyo kutokana na majeraha ambayo yamekuwa yakimsumbua kwa muda mrefu.

No comments:

Post a Comment