Friday, April 13, 2012

MARADONA AMKEJELI PELE.

KOCHA wa klabu ya Al Wasl, Diego Maradona amekejeli kauli ya nguli wa soka wa zamani wa Brazil Pele kufuatia kauli yake aliyoitoa kuwa mshambuliaji wa klabu ya Santos, Neymar ni bora kuliko nyota wa Barcelona, Lionel Messi. Pele alikiri wakat akihojiwa Jumanne kuwa Messi ni mchezaji mkubwa lakini alisisitiza kuwa mshambuliaji huyo bado hajamfikia kinda huyo wa Santos. Akihojiwa kuhusiana na suala hilo Maradona alishangazwa na kauli ya nguli huyo wa zamani na kusema kuwa kama Neymar ni mchezaji bora wa dunia wa kwasasa, Messi yeye atakuwa anatokea sayari nyingine. Wachezaji wote wawili walikuwemo katika tuzo za wachezaji bora wa dunia ambazo huandaliwa na Shirikisho la Soka Duniani-FIFA zilizofanyika Januari mwaka huu ambapo Messi ndiye aliyeibuka kinara wa tuzo hizo kwa mwaka 2011, wakati Neymar alipata tuzo ya goli bora la mwaka.

No comments:

Post a Comment