Friday, April 13, 2012

BALOTELLI ASISITIZA KUBAKIA CITY.

MSHAMBULIAJI wa Manchester City, Mario Balotelli ameeleza nia yake ya kubakia katika klabu hiyo licha ya meneja wake Roberto Mancini kupanga kumuuza mchezaji huyo mwishoni mwa msimu huu. Kadi nyekundu ya nne aliyopewa Balotelli ndani ya misimu miwili kwenye klabu hiyo, imemkatisha tamaa Mancini juu ya nidhamu ya mchezaji huyo, lakini wakala wake, Mino Raiola amesema mteja wake anataka kubaki Eastlands. Akihojiwa kuhusiana na uwezekano wa mchezaji huyo kurejea nchini Italia, Raiola amesema kuwa huu si wakati wa mchezaji huyo kurudi Italia ni lazima mchezaji huyo aendelee kujifunza nchini Uingereza. Kadi nyekundu ya mwisho ya Balotelli alipewa mwishoni mwa wiki iliyopita wakati City ikilala kwa bao 1-0 dhidi ya Arsenal baada ya kupewa kadi ya pili ya njano.

No comments:

Post a Comment