RAIS wa Shirikisho la Soka la Ulaya-UEFA, Michele Platini amesema kuwa michuano inayofuata ya Ulaya mwaka 2016 haitarajiwi kupungua ubora wakati watakapoongeza timu na kufikia 24 badala ya 16 kama ilivyo hivi sasa. Platini amesema kuwa kuongezeka kwa timu nane hakutakuwa na tatizo lolote katika michuano hiyo ya 2016 ambayo itafanyika Ufaransa, kutokana na hali aliyoiona katika michuano inayoendelea Poland na Ukraine hivi sasa. Michuano ya Ulaya ya mwaka huu imetoa mabao mengi na burudani ya kutosha katika michezo 22 zilizochezwa ambapo mpaka timu zikielekea katika hatua za mwisho za makundi hakuna timu hata moja zilizotoka sare ya bila ya kufungana. Platini aliongeza kuwa wanaweza kuongeza timu zingine nane na pia kuwa na hatua ya timu 16 bora katika michuano hiyo ili kuongeza ladha zaidi ya michuano hiyo kwa mwaka 2016.
Tuesday, June 19, 2012
PLATINI KUIKINGIA KIFUA EURO 2016 KUWA NA TIMU 24.

Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment