Monday, June 25, 2012

SAUDI ARABIA YARUHUSU WANAWAKE KUSHIRIKI OLIMPIKI.

Baadhi ya wachezaji wa kikosi cha timu ya taifa ya mpira wa kikapu ya wanawake ya nchi hiyo wakiwa katika picha ya moja  Machi  25 mwaka huu.
UBALOZI wa Saudi Arabia nchini Uingereza umesema kuwa wanamichezo wanawake wa nchi hiyo wataruhusiwa kushiriki michuano ya Olimpiki itakayofanyika jijini London kwa mara ya kwanza katika historia ya michuano hiyo. Mpaka sasa Saudi Arabia ni moja kati ya nchi tatu ambazo haziruhusu wanawake kushiriki katika michezo ambapo nchi nyingine ni Qatar na Brunei ambazo nazo pia zimepanga kupeleka wanamichezo wanawake katika michuano hiyo inayotarajiwa kuanza Julai 27 mwaka huu. Katika taarifa yake wakati wa kutangaza uamuzi huo, ubalozi huo umesema kuwa serikali ya kifalme ya nchi hiyo umeoamua kuruhusu wanamichezo wanawake kushiriki michuano hiyo baada ya kutambua mchango wake ambao unajenga maadili bora, urafiki na heshima kati ya nchi na nchi. Uamuzi huo ni nadra kutolewa na serikali ya nchi hiyo ambapo wanawake hawaruhusiwi kuendesha magari na pia hawaruhusiwi kupiga pamoja na kuongoza ofisi za umma ingawa sheria hizo nazo zinatarajiwa kubadilishwa ifikapo mwaka 2015. Wanawake wa Saudi Arabia pia hawaruhusiwi kuolewa, kusafiri nje ya nchi hiyo, kwenda shule au kufungua akaunti ya benki mpaka wawe na usimamizi wa mwanaume ambaye anatakiwa kuwa baba yake au mume wake.

No comments:

Post a Comment