Tuesday, April 3, 2012

VILLA'S PETROV IN POSITIVE MOOD.

NAHODHA wa klabu ya Aston Villa, Stiliyan Petrov yupo katika hali nzuri kiakili kabla ya kuanza kwa matibabu yake ya kansa ya damu mwishoni mwa wiki iliyopita. Mchezaji mwenzake ambaye walicheza wote katika klabu ya Celtic, John Hartson amesema kuwa afya aliyokuwa nayo mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32 raia wa Bulgaria itamsaidia kupambana na ugonjwa huo unaomkabili. Mchezaji huyo anaamini kuwa Petrov atakiruka kiunzi hicho kigumu katika maisha yake kwa kuwa nguvu anazo na anajua kuwa ulimwengu wote wa soka uko nyuma yake katika kipindi hiki kigumu. Hartson ambaye nae alifanikiwa kupambana na ugonjwa wa kansa ya pumbu ambayo kitaalamu inaitwa Testicular mwaka 2009 amesema kuwa aliongea na Petrov Jumapili kabla hajaanza kupata matibabu katika Hospitali moja inayoshughulika na magonjwa hayo iliyopo jijini London na kwamba yuko katika hali nzuri.

No comments:

Post a Comment